Jumanne, Julai 17, 2012

SIMULIZI YA MAMA MDOGO SURA YA ....10...

  KITABU MALIPO NI HAPAHAPA
MTUNZI ADELA DALLY KAVISHE
ILIPOISHIA.....Mama mdogo alibaki amejiinamia katika meza akifikiria namna ya kumpata Jamal kwani mbinu ya kwanza ilishashindikana.
"Mh huyu Jamal anajidai mjanja sana kuliko mimi nitampata tu siwezi kumuacha namuhitaji sana.” Aliwaza mama mdogo huku akiondoa chakula mezani na kupeleka jikoni.

 
INAPOENDELEA,......Mama mdogo aliendelea kumfuatilia na kumfanyia vitimbwi Jamal ilimradi tu ampate. Wakati mwingine mama mdogo alikuwa akimfuata Jamal usiku akiwa amelala na kugonga mlango lakini Jamal alikuwa hafungui. Jamal alijitahidi sana kumkwepa mama yake mdogo.

Siku moja wakati Mzee Said hayupo mama mdogo alimfuata Jamal chumbani kwake na kisha kumkumbatia kwa nguvu huku akiwa amevaa nguo iliyomuacha wazi sehemu kubwa ya mwili wake.

“Jamal usinitese hivyo nakuhitaji mpenzi.” Aliongea mama mdogo kwa sauti ya mahaba huku amemkumbatia Jamal. Jamal alimshika na kumsukuma kwa nguvu.
“Mama mdogo nakwambia tena sikutaki kwa nini unapenda kunifuatafuata naomaba uniache.” Alilalamika Jamal.
“Sikiliza nikwambie Jamal, wewe unajiona mjanja tutaona nani zaidi kati yangu na wewe. Fahamu kwamba mimi ndio mother house (mama mwenye nyumba) wewe nenda utanifuata mwenyewe.” Alifoka na kuondoka mama mdogo akimwacha Jamal akiwa na mawazo mengi juu ya vituko anavyofanyiwa.

“Lakini haya yote amesababisha baba, hata nikienda kumwambia mambo anayonifanyia mama mdogo anaweza asiniamini. Sina raha kabisa katika nyumba hii.” Aliwaza Jamal, kisha akaondoka kwenda kwa marafiki zake.


Jamal aliporudi nyumbani alimkuta baba yake akiwa amerudi kutoka kazini akiwa amekaa sebuleni na mke wake, alimsalimia baba yake na kuelekea chumbani. Wakati anaondoka mama mdogo alimwangalia sana kwa macho yaliyojaa hoja nyingi.

“Unajua mume wangu Jamal siku hizi anachelewa sana kurudi nyumbani, sijui ni kwanini.” Alisema mama mdogo. Mzee Said bila hata kuhoji wala kufanya uchunguzi juu ya tuhuma za Jamal alihamaki na kuonyesha uso wa hasira.

“Hebu mwite haraka.” Alitoa amri Mzee Said.
Mama Mdogo alitoka haraka kumwita Jamal ambaye alimkuta amejilaza kitandani kwake. Alipomweleza kuwa anaitwa alinyanyuka haraka na kwenda kusikiliza wito wa baba yake.
“Hivi wewe Jamal hii tabia ya kuchelewa kurudi nyumbani umeianza lini? Si nilikwambia sitaki hapa nyumbani kwangu,haya nataka uniambie umetoka wapi?” Jamal alinyamaza kimya kwa muda kisha akamjibu baba yake.
“Sikuwa mbali na nyumbani baba”
“Usiniambie habari za hukua mbali na nyumbani, umeanza tabia mbaya na hao marafiki zako sitaki kuwaona hapa kwangu sawa?” Alifoka Mzee Said huku akigeuka kumwangali mkewe.

“Unajua haya makundi ya vijana, wengi wao wanavuta bangi na kudanganyana tu hakuna lolote la maana wanalofanya." Alitamka mama mdogo huku akimwangalia Jamal kwa dharau.
“Haah! We mama mdogo! unaongea nini? Ni lini ulituona mimi na wenzangu tunavuta bangi? Acha roho mbaya mama.” Alifoka Jamal kwa hasira bila hata kujali uwepo wa baba yake.

Baba yake kuona vile alinyanyuka na ku mpiga Jamal kibao cha usoni. Kama hivyo haitoshi alichukua mkanda na ku mpiga sana huku akitamka maneno makali.
“Ni tabia gani uliyoianza? Yaani unamjibu mama yako hivyo? Nitakuua leo mjinga kabisa we! Na ukiendelea na tabia hii nitakufukuza hapa nyumbani umekuwa na tabia mbaya sana.” Alifoka Mzee Said huku akiendelea kumchapa sehemu mbalimbali za mwili na mkanda wake wa suruali.

 Jamal alilia sana, huku akimkumbuka marehemu mama yake. Hata hivyo aliamua kumwomba msamaha baba yake pamoja na mama yake mdogo, halafu akaelekea chumbani.
“Laiti mama angekuwepo haya yote yasingetokea, yaani baba ananipiga kwa sababu ya huyu mwanamke inaniuma sana.” Aliwaza Jamal na kuhuzunika sana.nini kinaendelea usikose sura ya 11.......

Maoni 3 :

Bila jina alisema ...

Yani hapo hkna jinc itabd tu jamal hamkubali kero zikizd.dah pole cna jamal kubal kula mzgo lkn.

emuthree alisema ...

Malipo ni hapahapa duniani, kwa mungu anakwenda kufungiwa mahesabu!

Bila jina alisema ...

Kwa kweli Jamali rafiki yetu hapo hakuna ujanja itabidi upite naye masuala ya shule yanyooke.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom