Jumatatu, Julai 09, 2012

"MAPENZI HAYAANGALII UMRI" NYOTA WA LEO MARIAH CAREY

Mariah Carey (amezaliwa tar. 27 Machi1970) ni mwanamuziki, mtunzi, mtayarishaji na pia ni mwigizaji wa Kimarekani. Alitengeneza albamu yake iliyofanya vizuri katika masoko mbalimbali na chati mbalimbali mwaka 1990, chini ya studio ya Columbia Records chini ya Tommy Mottola na kuwa mwanamuziki wa kwanza wa kike kufikisha wimbo katika nafasi ya kwanza nchini Marekani

Mariah  mwenye umri wa miaka 42  na Muigizaji  Nick Cannon, mwenye umri wa miaka 31 walifunga ndoa Aprili   30, 2007 nchini Bahamas. Carey na Cannon walipata watoto mapacha wao wa kwanza  wa kike anaitwa Manroe na wa kiume anaitwa Moroccan April 30, 2011 katika hospitali ya  Los Angeles

Tofauti kubwa ya umri iliyopo baina yao imekuwa ikizua maneno  tangu wawili hao walipooana wengine wamekuwa wakimshutumu kijana huyo kuwa amefuata mali kwa mwanamama huyo mwenye utajiri mkubwa unaokadiriwa kuzido dola milioni 225 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 300 ambazo zimemfanya atese mara kwa mara katika chati za wanamuziki wa kike matajiri zaidi duniani. 

Maneno ya watu kuhusiana na uhusiano wao hazionyeshi kuteteresha uhusiano wao  kwani bado wanaendelea kufurahia ndoa yao. Mariah  Carely ndoa yake ya kwanza alifunga na mmiliki wa lebo ya kurekodi  muziki ya Sonny Tommy Mottola mara kwa mara amelazimika kukanusha mahusiano na rapa mtukutu  Eminem ambaye amekuwa akidai kuwa waliwahi kuwa wapenzi

Malumbano ya Eminem na Mariah yaliendela hadi  kuamua  kuandika wimbo wa kumponda mwenzake  wimbo unaoitwa OBSSSED ambapo katika video yake anatokea kijana anayevaa OPP, kama Eminem akimfuata fuata Mariah kila aendako. Cannon naye alishawahi kusema kwamba atamfanyia kitu Mbaya rapa Eminnem ambaye jina lake halisi ni Marshall Mathers.

Mariah na Cannon siku ya ndoa yao haijalishi umri hapa ni mapenzi tu 

Maoni 1 :

emuthree alisema ...

Cha muhimu hapo ni mapenzi, mnaweza mkaoana umri sawa lakini mapenzi yakawa na tofauti mara mbili yenu, hakuna amani.
Hata hivyo hebu muangalia huyu Cery menyewe utafikiri ana umri sawa na huyu `baby-boy' wake!
Safi sana kupendana mkiwa mumepishana umri, maana uzoefu wa siku nyingi plus wa karibu mnakuwa mbali sana!
Au unasemaje mpendwa?

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom