Jumatatu, Desemba 27, 2010

"Sikutegemea kama ningekuja kumfumania mume wangu na mdogo wangu imeniuma sana" mama Rozi wa Kimara.

Hii ni picha ya moja kati ya wanandoa wakifurahia ndoa yao..Ndoa ni furaha, amani, na upendo kwa uelewa wangu nimepata ujumbe huu "Habari yako Adela naomba unisadie nipate ushauri kutoka kwa watu mbalimbali kupitia blog yako mimi ni mwanamke nimeolewa nina watoto watatu katika maisha yetu ya  ndoa tumeishi kwa furaha sana kiasi kwamba sikutegemea kama ningekuja kumfumania mume wangu akiwa na mdogo wangu ambaye nilikuwa nikiishi naye nyumbani siku ya tukio nilikuwa nyumbani jirani yangu akanipigia simu na kuniambia amemuona mume wangu na mdogo wangu wakiingia hotelini na kuniambia niendenikajionee mwenyewe kiukweli nilipofika nilichokiona sintokaa nisahau nilimkuta mdogo wangu akiwa anaogelea katika swiming pool na mume wangu huku wakiwa wamekumbatiana nilihisi kuishiwa nguvu na moja kwa moja nilimshika mdogo wangu nakuanza kumpiga kwa uchungu  nililia sana baadae mume wangu ananiomba msamaha na kusema kuwa shetani alimpitia mimi nataka niondoke naona aibu kuendelea kuishi naye inaniuma sana na mdogo wangu amekimbia sijui hata alipo"...mmmmh jamani tamaa gani hizi ushauri wako mdau.........

Maoni 9 :

Yasinta Ngonyani alisema ...

Mama weee! kwa kweli ningekuwa mimi nadhani ningezimia kabisa yaani mume wangu na mdogo wangu. Yaani ningechanganyikiwa je ni nani alianza na ni muda gani wamekuwa wakifanya hivyo? Ushauri wangu ningewaacha na nisingewaamini tena wote wawili hasa mume wangu.Pole saba dadangu , maisha haya jamani......

Bila jina alisema ...

huyo mdogo wako anaumri gani kwanza tujue alidanganywa au alitaka kwa N zake

Unknown alisema ...

Nami uchungu umeniingia baada ya kusoma sakata hili. Pole sanan Dada yangu.Jipe muda, kaa chini utafakari kidogo hasa juu ya maisha yenu ya ndoa. Ona wazee mshauriane kabla ya kufanya maamuzi yoyote.

Bila jina alisema ...

Pole sana dada yangu inauma sana lakini kabla ya yote mwombe mungu akupe njia, kwani yeye ndiye muweza wa yote. hakuna kimshindacho yeye ukimwamini.

Bila jina alisema ...

Pole sana jipe moyo wengi yametupata hayo katika maisha ya ndoa, lakini ushari wangu kama dada yako naomba usimuachie mdogo wako akaendeleza ndoa yako utaumia zaidi hawa watoto hiyo ni aibu yake wewe endelea na mume wako akatafute wake ashindwe kabisa na apotee wanaume wote hao akamuone wako tu mtoto mbaya huyu usimwachie kaza buti jiulize wapi umelegalega rekebisha songa mbele na mungu akubariki sana inauma sana jamanii aaaa

sam mbogo alisema ...

dada zangu sijui nimechelewa,kutowa mawazo.kwanza pole sana.hapa tatizo siyo mdogo wako,tatizo ni mumewako.sasa angalia nini kilisababisha jamaa aduu na mdogo wako,pia ongea na mdogo wako kwa upole kwani mambo ya sha haribika,waweza jifunza kitu ukiongea vizuri na mdogo wako.na mwisho,mume akiombaradhi msamehe,na angalia mbele,yawezekana shetani alipita tu.ila pata funzo ,moja kutoka kwa mdogo wako, na pili kutoka kwa mumeo. kaka s.

Bila jina alisema ...

sorry nimechelewa kupost but pole sana ndugu yangu! huyo mumeo muongee muyamalize maana mmeshazaa watoto watatu! na mdogo wako arudi kwao kwa wazazi na akajitegemee! km hatarudi kukuangukukia msahau maana alijua anachofanya ! shemeji yake angekuwa anamsumbua angekwambia

Bila jina alisema ...

sorry nimechelewa kupost but pole sana ndugu yangu! huyo mumeo muongee muyamalize maana mmeshazaa watoto watatu! na mdogo wako arudi kwao kwa wazazi na akajitegemee! km hatarudi kukuangukukia msahau maana alijua anachofanya ! shemeji yake angekuwa anamsumbua angekwambia

Bila jina alisema ...

wote wana makosa,huyo mume wako mpe talaka,

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom