Ijumaa, Aprili 06, 2012

Nyota wa leo Michelle Obama

Michelle LaVaughn Obama (jina la kuzaliwa ni Michelle LaVaughn Robinson), amezaliwa mnamo tar. 17 Januari, 1964) ni Mwanasheria wa Kimarekani na ndiyo mke wa Rais wa Marekani Bw. Barack Obama. Huyu ndiye Mwafrika-Mwamerika wa kwanza kuwa Mwanamke wa Kwanza wa Marekani.

Michelle alizaliwa na kukulia kitongoji South Side ya Chicago na kusoma hadi kuelekea katika Chuo Kikuu cha Princeton halafu baadaye katika Kitivo cha Sheria cha Harvard.Baada ya kumaliza elimu yake hiyo, alirudi Chicago na kukubali kuchukua nafasi ya kazi katika kampuni ya Sidley Austin, halafu baadaye akaja kuwa kama mmoja kati ya wafanyakazi wa meya wa Chicago Bw. Richard M. Daley, halafu baadaye akafanya kazi katika Chuo Kikuu cha Chicago na Hospitali za Chuo Kikuu cha Chicago.



Michelle Obama ni dada wa Craig Robinson, kocha wa mpira wa kikapu wa Oregon State University. Alikutana na Barack pale alipojiunga na Sidley Austin. Pale Barack Obama alipochaguliwa kuwa kama Seneta, familia ya Obama ikachagua kuishi mjini Chicago South Side kuliko kuishi mjini Washington, D.C.

FIRST LADY

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom