Jumatano, Novemba 07, 2012
SIMULIZI YA MAMA MDOGO SURA YA .....13.....
KITABU MALIPO NI HAPAHAPA
MTUNZI ADELA DALLY KAVISHE
ILIPOISHIA Baada ya maongezi hayo Goodluck aliaga na kuondoka kuelekea kwao akimwacha Jamal akiwa na mawazo mengi kuhusu mama yake mdogo. Siku iliyofuata yapata saa nne asubuhi wakati babake akiwa kazini Jamal alimfuata mama yake mdogo sebuleni ili azungumze naye kuhusu swala la kupekekwa shule. Alipoingia tu alimkuta amekaa katika sofa akifuma kitambaa.
INAPOENDELEA:
“Habari
za asubuhi mama mdogo? Alisalimia Jamal. “Nzuri
Jamal umeamkeje? Ah! Salama kabisa” Alijibu Jamal. “Vipi
Jamal mbona unaonekana mnyonge sana, unaumwa?”Aliuliza mama mdogo. “Hapana
mama mdogo, nina shida na wewe.” Alisema Jamal. “Heeh!
Makubwa na wewe huwa unashida? Haya hebu sema unashida gani?”
Alishangaa na kuuliza mama mdogo kwa kebehi. Unajua
mama mdogo mimi napenda sana kusoma, baba anaonyesha hataki
tena kunisomesha. Lakini ninauhakika nikikutumia wewe anaweza kubadili
msimamo wake. Tafadhali naomba unibembelezee.” Alitamka Jamal. “Jamal
tatizo siyo baba yako hataki kukupeleka shule. Ila tatizo ni wewe mwenyewe
hutaki kwenda shule.” Alisema mama mdogo huku akiweka kitambaa juu
ya meza na kusogea kwa Jamal.
“Hapana
mama mdogo mimi shule napenda sana.” Alijibu Jamal. “Hapana
kama unapenda shule usingekuwa unanikatalia ombi langu siku zote
hizi.” Aliongea mama mdogo huku akirembua macho. “Jamal
mimi nakupenda sana na unajua fika kwa nini unakataa ombi langu?
Hivi huoni kama unateseka bure kwa ujinga wako?” Aliuliza mama
mdogo. Jamal
alinyamaza kimya kidogo huku wakiangaliana na mama mdogo.
Mama mdogo
alitabasamu kimahaba kisha akaangalia chini kwa aibu. “Unajua
mama mdogo hilo ni jambo la hatari sana, baba akigundua ataniua.”
Alitahadharisha Jamal.
MANENO MATAMU KWA MPENZI
MWANAMUZIKI RAY C ANAHITAJI MSAADA WAKO MDAU
Kutokana na kuwa na matatizo ya kuathirika na madawa ya kulevya Ray c msanii wa bongo fleva anahitaji msaada wako ili kupata matibabu ya kuondokana na tatizo hilo |
kiuno bila mfupa RAY C ukweli ni kwamba amekiri makosa ya kutumia madawa ya kulevya na hivyo kwa sasa anahitaji msaada KUTOA NI MOYO |
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)