Ijumaa, Oktoba 11, 2013

CHANGAMOTO NYINGI ANAZOKUTANA NAZO MTOTO WA KIKE NI CHANZO CHA KUTOTIMIZA MALENG0 YAKE

 Ikiwa leo ni maadhimisho ya mtoto wa kike duniani kauli mbiu mwaka huu  inasema “Kuwawezesha wasichana, kuhakikisha haki zao za binadamu na kushughulikia ubaguzi na unyanyasaji dhidi yao ni muhimu kwa maendeleo  na kwa ajili ya familia nzima ya wanadamu.” 

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa Tanzania  ni miongoni mwa nchi zenye viwango vya juu vya ndoa za utotoni duniani. 


Ndoa za utotoni ni miongoni mwa mambo yanayomkwaza mtoto wa kike nchini pamoja na mambo mengine, ashindwe kupata elimu ambayo ndiyo msingi wa maisha. Takwimu zinaeleza kuwa kwa wastani, watoto wawili kati ya watano huolewa kabla ya kutimiza umri wa miaka 18.
Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa asilimia kubwa ya vifo vinavyotokana na uzazi, huwapata wasichana wanaoolewa katika umri mdogo.

Ni kutokana na sababu hizi na nyingine nyingi, sisi tunaposisitiza kuwa mtoto wa kike ana haki zote za kuthaminiwa kama ilivyo kwa mtoto wa kiume, hivyo apewe mambo yote ya msingi ikiwamo elimu.



Kwa bahati nzuri, baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali yameungana kufanya kampeni ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake ukiwamo wa ndoa za utotoni. MTO WA KIKE ASIBAGULIWE KATIKA ELIMU. 



Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom