Jumatatu, Machi 03, 2014

MIGOGORO KATIKA FAMILIA, NA UKATILI DHIDI YA WATOTO NI BAADHI YA MAMBO YANAYOKWAMISHA USTAWI WA WATOTO

 Watoto wengi wamejikuta  katika maisha ya kutangatanga  hasa baada ya ndoa nyingi kuvunjika kutokana na migogoro katika familia .Migogoro katika familia, unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto,  ni mambo ambayo yanasababisha watoto kuishi kwa hofu miongoni mwa jamii
Watoto wanaoishi katika mazingira magumu wanakutana na changamoto nyingi sana, kama ubakaji, kuharibika kisaikolojia, kukosa elimu, kukosa haki za msingi na mengineyo mengi ambayo ni muhimu kwa mtoto ni vyema jamii ikalitambua jambo hili kwa mapana zaidi na kuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia watoto kutimiza malengo yao ikiwa ni pamoja na kupata haki zote za msingi.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom