Alhamisi, Septemba 30, 2010

Daktari mzuri katika hospitali yoyote ni yule aliyemcheshi,,asiye na hasira na kujali kila mgonjwa bila kubagua..

Unapoenda Hospitalini na kukutana na Daktari au Nesi ambaye ni mkarimu inaleta faraja sana,,kwani kuna baadhi ya manesi au madaktari ambao sio wakarimu wanaangalia kipato,,kama hauna basi kutibiwa kwako kunakuwa kwa shida sana,,jamani sio vizuri sisi sote ni binadamu ambao ni ndugu aliyenacho na asiyenacho,,hatuna budi kusaidiana,,mara ngapi tunasikia vifo vya watoto wadogo,,au vya kina mama wajawazito kutokana na uzembe wa manesi na madaktari.

 kutokana na hali kama hizo siku hizi unakuta watu wanachagua hospitali za kwenda kupata huduma,,hususani kwa wale wanaojiweza mtu unakuta anaye daktari wake maalumu kwa ajili ya kumtibu,,sasa je sisi wa hali ya chini nani wa kutuangalia jamani tunawaomba madaktari na manesi watusaidie ijapokuwa wanakutana na matatizo mengi katika kazi zao au wakati mwingine wagonjwa labda pia wana kero zao,,kibinadamu ushirikiano ni mzuri baina ya mgonjwa pamoja muuguzi......

Maoni 6 :

o'Wambura Ng'wanambiti! alisema ...

...only if they exist... kwa kuwa manesi na madaktari wengi wa siku hizi wamepinda san :-(

Yasinta Ngonyani alisema ...

Mmmmhh!! kaka chacha unamaanisha nini wamepinda san?

Hashir alisema ...

Kwanza mtu unapokuwa mgonjwa, it means wewe unahitaji mtu wa kukusaidia katika hali zote, sasa hawa wauguzi katika hospitali zetu nyingi za serikali, wanakuwa na mambo kama haya, yaani sijuwi wanajionaje au wanafikiria wao watakuwa hawaumwi... maishani mwao, hii tabia ya wauguzi kudharau wagonjwa ipo sana na inafaa kukemewa na viongozi wetu wa serikali, coz inarudisha nyuma upendo baina ya jamaa wa mgonjwa na mgonjwa mwenyewe kwa wauguzi, tabia hii sio saaana kwa hospitali za binafsi, coz wenye hospitali hizo wanakuwa wakali sana, na wanataka huduma njema kwa wagonjwa ili wao wapate wateja wengi, sasa kama serikali yetu na wao hawajawa wakali katika hospitali zao, basi tabia hii itazidi kuendelea, but nawapongeza muhimbili kitengo cha kutoa damu, coz nilienda pale sikumoja nikahudumiwa vizuri tu na wale watoaji damu big up kwao!!!

o'Wambura Ng'wanambiti! alisema ...

da Yasinta, wamepinda manake wengi wao hawana wito wa unesi na udaktari kama zamani

ADELA KAVISHE alisema ...

@Chacha inawezekana ikawa kweli kwani sio wote waliosomea udaktari au unesi wana wito huo wengine utafikiri wamelazimishwa@Yasinta tuko pamoja mpendwa@Hashir asante sana binadamu tunatofautiana jamani

Devota Sotel alisema ...

ni kweli kabisa tuko pamoja,,,

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom