Jumanne, Septemba 28, 2010

Jamaa limembaka denti na kumpa ujauzito,,eti linasema shetani alimpitia,,kweli jamani,

Mabinti kama hawa pichani wanakutana na matatizo mengi sana likiwemo la ubakaji,,,,,kuna kijana mmoja mkazi wa Kinonko wilaya ya Morogoro Ramadhani Benjamin(23) amehukumiwa miaka 30 jela kwa kitendo cha kumbaka binti wa miaka 16  mwanafunzi wa darasa la sita,,na katika kujitetea mahakamani kijana huyo alisema shetani alimpitia hakukusudia kufanya hivyo,,

Vitendo vya ubakaji ni vitendo vilivyokithiri sana katika jamii yetu huku vikiongezeka kila kukicha,,sijui ni kwanini watu wanakuwa hawana hata chembe ya huruma kufanya vutendo vya kikatili kama hivi,,inauma sana,,,,,,,,,,tena wengi wao wanamsingizia shetani,,

Maoni 5 :

Yasinta Ngonyani alisema ...

Shetani alimpitia? Yaani hili swala sijui litaisha lini? wanawake wote hawa mpaka ukambaka binti wa miaka 16 na kumharibia maisha yake KWANINI halafu anasema alipitiwa na shetani. Au labda yeye ndiye shetani mwenyewe.. Swala kama hili huwa linaniumiza sana roho kiasi kwamba ....basi naacha..

ADELA KAVISHE alisema ...

@Yasinta asante mwaya tuko pamoja ,,yaani ni tamaa tu na ulimbukeni hakuna cha shetani,,kama ulivyosema labda yeye ndiye shetani,,haya matatizo yapo kila kukicha kilichobaki ni kumrudia Mungu..

Yasinta Ngonyani alisema ...

Na natamani hiyo miaka thelathini aozee hukohuko unajua nimechoka kusikia haya mambo hebu angalia hapa http://www.youtube.com/watch?v=Reuaia3f_Nc au http://matondo.blogspot.com/2010/09/sidanganyiki.html

emu-three alisema ...

Shetani atasingiziwa mengii sasa. Siku ya hukumu atatushangaa sana, atasema `mbona huyu binadamu kafanya mengi ambayo hata sisi hatuyajui...ajabu kabisa

Lawyer J Bokilo alisema ...

Watu wamekosa aibu, wanamsingizia shetani wakati wao ndio mashetani, sijui kwa nini mtu hafikirii madhara yatakayotokea kutokana na unyama wake?

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom