Jumatatu, Septemba 20, 2010

Kitendo cha kumuuliza mpenzi wako, je unanipenda?? kila wakati mkiwa pamoja ni sawa na kutokujiamini.

Mwanzoni kwenye mahusiano baina ya wapenzi huwa kuna maswali kama haya je unanipenda kwa kiasi gani? na yote ni kufahamu kiasi cha upendo alionao mwenzio juu yako,na wengine huuliza kwa nini umenipenda na majibu yake huwa katika hali ya utofauti kwani kila mtu anajua kile anachokipenda kutoka kwa mwenzake..mwingine atapenda sura,macho,umbo lakini pia kikubwa zaidi wengi huangalia tabia je huyu mtu ana tabia zinazostahili,ikiwa ni moja kati ya nguzo muhimu katika mahusiano..

Baada ya kufahamu ni kwa kiasi gani mnapendana basi inakuwa ni furaha na kufurahia penzi lenu,wote kwa pamoja,,lakini sasa kuna ile hali ya kutojiamini hususani kwa upande wa wanawake utakuta mwanamke anamuuliza mpenzi wake mara kwa mara unanipenda kweli? huku swali hilo likijirudia kila mnapokutana,wanaume wengine hukasirika kutokana na maswali kama haya muhimu ni kujiamini na kama anakupenda utaona vitendo na si kwa kutamka tu kwa maneno..kwani anaweza kusema anakupenda lakini moyoni hana mapenzi na wewe.....

Kama mwenzio anakupenda na wewe unampenda hakuna haja ya kuwa na wasiwasi katika mapenzi kinachotakiwa ni kuongeza juhudi kujenga uhusiano ulio bora,jaribu kuepuka mambo ambayo yanaweza kuwa kero katika mahusiano yenu kwani ndio chanzo cha migogoro ya hapa na pale.kwa kushirikiana jengeni uhusiano uliojaa mahaba mazito na amani.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom