Ijumaa, Septemba 17, 2010

Leo ndani ya Big brother all stars Mwisho asema watu wanaoendesha magari huku sauti ya muziki ikiwa juu ni kero....

Mwisho akiwa na mpenzi wake Merly mshiriki kutoka Namibia, ndani ya Jumba la Big brother na pembeni ni Uti mshiriki kutoka Nigeria,leo Mwisho na Uti walikuwa wakibishana kuhusu watu wanaoendesha Magari barabarani na kuweka sauti kubwa ya muziki, Mwisho alikuwa akisema kufanya hivyo ni kero kubwa kwa watu wengine kwani kama unapenda kusikiliza muziki basi sikiliza kwa faida yako na si kuweka sauti kubwa kama vile upo disko..

Uti yeye hakukubaliana na yale aliyokuwa akisema Mwisho alimpinga na kusema kila mtu anayo starehe yake na hakuna kero yeyote kupiga muziki kwa sauti hata Merly ,mpenzi wake na Mwisho aliungana na Uti na kumpinga Mwisho.mjadala ulikuwa mkubwa hadi kufikia hatua ya Uti kumuita Mwisho bado mtoto mdogo na ni mshamba angekuwa anaishi mjini angekuwa mjanja,na kumshauri ahamie mjini,wakati huo huo Mwisho naye akamwambia Uti utoto ndio unamsumbua ndio maana hamuelewi.lakini Uti na Mwisho ni marafiki na pia wapo katika group moja mjengoni humo la Midnight crew.

Mambo ya Big brother all stars hayo,,,je wewe unaonaje mjadala huu...
Mwisho Mwampamba katika pozi mpigie kura andika VOTE kisha andika MWISHO tuma kwenda namba 15726 tumpigie kura ndugu yetu......

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom