Jamani duniani kuna mambo....kuna jamaa watatu walifanya dili wakapata zaidi ya milioni 900.Kutokana na kuwa walikuwa ni marafiki waliamua kwenda kujificha porini ili ishu itulie town..wakaaa porini kwa muda wa miezi mitatu.katika kipindi chote hicho walikuwa wakila mikate na maji ya mtoni ingawa walikuwa na pesa kibao hizo milioni 900....sasa siku moja mikate iliwaishia ikabidi wamtume mwezao town kununua mikate...jamaa akakubali,akavaa kofia kubwa,koti pamoja miwani akajitupa town kununua mikate na alifanya hivyo ili asijulikane..Alivyofika town jamaa akafikiria kuwa bora mikate atakayonunua aweke sumu kisha yeye ale kabisa na akirudi awaambie wenzake kuwa yeye ameshakula chakula hivyo wakila mikate wafe achukue pesa zote asepe...kumbe jamaa nao porini wakawa wanajadiliana kuwa jamaa akirudi wamuue ili wagawane pesa wawili tu na wakati huo jamaa town naye mikate yote akawa ameiwekea sumu pamoja na juice....jamaa akaanza safari ya kurudi porini kwa jamaa zake huku akiwa na imani kuwa atachukua pesa zote maana watakufa kwa kula chakula chenye sumu hivyo hivyo kwa jamaa zake....jamaa akafika porini kama kawaida baada ya kutembea muda mrefu,kumbe wakati anafika jamaa nao walikuwa wanamsubiri wammalize...alipofika tu wakamdaka wakamnyonga akafa.....jamaa wakashauriana kuwa kwa kuwa jamaa ameshakufa basi wale chakula kisha wasepe...wakala chakula pamoja na juice na haikupitamuda nao wakafa hapo hapo....milioni 900 zikabaki bila ya mwenyewe zaidi ya kuliwa na mchwa........TAMAA MBAYA
by Njenga
Maoni 2 :
hahahahaha nimeipenda sana hii mpe hi njenga....
daaah njenga kwa vituko,,nimeipenda Adela big up blog itakuwa juu sana
Chapisha Maoni