Alhamisi, Septemba 23, 2010

Uvumilivu katika mahusiano ni muhimu sana,,lakini pia una mwisho wake...

Unaweza ukawa unampenda sana mpenzi wako na kuvumilia makosa yote yanayojitokeza lakini kama akiwa ni mtu ambaye anatenda makosa halafu  hajifunzi kutokana na makosa anayoyafanya na kujirekebisha,,kila siku amekuwa akirudia makosa hayo hayo kiukweli inafikia kipindi mtu unachoka na kukosa amani  mwisho wake mapenzi yanaisha kwa yule uliyekuwa ukimpenda kutokana natabia alizonazo, mfano ni mlevi sana ,ni muongo,ana wapenzi wengi nk,,,jamani usimfanyie mwenzio kile ambacho hupendi kufanyiwa na wewe..jiulize kama ingelikuwa ni wewe ungejisikiaje..

Maoni 4 :

Bila jina alisema ...

Adela unajuwa kuwa mmoja kati ya marafiki ni lazima awe na guvu ya kuumba kitu kipya ndani ya mwenzie? Ninapo sema hivyo ninamaana kuwa: Kwanza unampenda rafiki kama alivyo, kwa jinsi ya matendo yake, muonekano wake na mwenendo wake, yawezekana na ndivyo ilivyo kwamba si mambo yote kwa mwenzio ni mema na yanakubalika kwako, hivyo unapo amua kumpenda na kujenga uhusiano kinachofuatia ni kumuondolea yale ambayo wewe yanakukera na kumvalisha utu unaoutamani wewe. Hili linawezekana pia kwa msaada wa Maombi kwa Mungu aliye kupa rafiki mzuri. Adela, mimi mtazamo wangu ni kwamba haisaidii kumwacha kwa sababu ya tabia yake, bali cha msingi ni kuondoa tofauti zilizopo miongoni mwa marafiki ili kuimalisha uhusiano kuliko kuvunja na kuwa na uhusiano mpya kila siku.

From your friend; Lazaro Kadili.

Bila jina alisema ...

inategemea unavumilia nini haiwezekani mtu anatembea na mtu mwingine alafu unavumilia nini ukiuliza atamsingizia shetani kwanini shetani asikukamate ukaenda kulima anakukamata unafanya mambo ya ajabu adela hv hili la sheteni tutamsingizia/mpaka lni

ADELA KAVISHE alisema ...

asante Lazaro lakini sijakataa ila inapotokea hali kama hii umeshindwa kuvumilia ndio mwanzo wa kukaa na kufikiri nikiingia tena katika uhusiano mpya nichague mtu sahihi ambaye hatoniumiza tena na kuna mambo mengine kiukweli hayavumiliki na hii ni kwa baadhi ya watu walioshindikana,,pia ndugu uliyesema wengine wanamsingizia shetani ni kweli ,,na hiyo tabia siipendi kweli ni bora kuwa muwazi kama umekosea jitambue omba msamaha na ukisamehewa jaribu kuwa makini usikosee tena....

Bila jina alisema ...

GREAT WORK

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom