|
Mama ni mtu wa muhimu sana katika maisha yetu,na katika hilo kina mama ulea watoto wao katika shida na raha sizani kama kuna mama anayependa mtoto wake ateseke kwa mama ambaye anapenda mwanae ateseke atakuwa si mtu mzuri katika jamii.Huko Wilayani Songea katika kijiji cha Ngahokola kuna kijana anatafutwa baada ya kumuua mama yake mzazi kwa madai kuwa mama yake alikuwa anamfanyia mambo ya kishirikina Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamhanda amesema tukio hilo limetokea jana saa 9:00 usiku na alimtaja aliyeuawa ni Dariel Moyo (56).
Amesema siku ya tukio mama huyo akiwa amelala nyumbani kwake aliuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na mtoto wake jina limehifadhiwa ambaye kwa muda mrefu amekuwa akimtuhumu mama yake kwamba homa inayomsumbua kwa muda mrefu inatokana na mama yake kumfanyia mambo ya kishirikina..baada ya kumuua mama yake mtuhumiwa amekimbia kusikojulikana amesema kamanda wakati akizungumza na gazeti Mwananchi na polisi wanaendelea kumsaka |
Jamani mama analea mtoto kutoka utotoni lakini mtoto akishakuwa mtu mzima kuna mengi yanayoweza kutokea,,lakini muhimu kuwaheshimu baba na mama katika maisha yetu,,sasa sijui nisemeje kuhusu huyo kijana labda niwasikilize wadau..
Maoni 2 :
Ukisikia laana ndiyo hii!
@Emu three umeonaeeeh
Chapisha Maoni