Tazama picha hii hawa wakina dada wakisutana,kwa asilimia kubwa wanawake walio wengi wanapenda kugombana na kuwekeana vinyongo,,kama kuchukiana,yaani kuwa maadui,nataka kusema ili kuondoa ugomvi n muhimu kumpenda adui yako kwani inakusaidia unaweza kuwa mwenye furaha zaidi kwa kufanya hivyo,pia utakuwa mfano mzuri wa kuigwa na jamii inayokuzunguka. |
Vilevile ugomvi wa wapenzi unaweza kuleta uadui baina ya wawili hao,sasa kutokana na kufahamu nani mwenye matattizo katika ugomvi unaweza kufahamu mbinu za kuishi naye,kwani unapoishi na kumpenda adui yako inakusaidia wewe maslahi yako kwa afya na kisaikolojia ijapokuwa ni vigumu kufanya hivyo kwa baadhi ya watu kutokana na hasira.ukimpenda adui yako pia hata hapo baadae yule adui atajiona yeye ndiye mjinga. |
Uadui unaweza kusababisha marafiki kupigana,,kutokana na ugomvi uliopo baina yao..ili kuepuka uadui unatakiwa kufungua moyo wako,,kudhibiti hisia za chuki,mchukulie adui yako kawaida usimuone kama shetani,na kubali yaliyotokea ili iwe rahisi kumsamehe na kuendelea kumpenda,wakati wa kufanya hivi pia tafakari yale mazuri aliyonayo adui yako,,kwani kila kibaya pia kina uzuri wake inawezekana adui yako ni muongo, au mgomvi lakini ni mtu mkarimu na ana heshima basi fikiria hayo ili kuonyesha upendo kwa adui yako ni vizuri na itakusaidia wewe kuweza kuishi na watu wa aina mbalimbali. |
Maoni 1 :
Ni kweli ugomvi unaleta uadui na pia kukasirika hupunguza busara. Lakini tukumbuke pia kuwa sisi ni binadamu na binadamu yoyote yule lazima atende baya/kosa. Upendo Daima!!!
Chapisha Maoni