Jumatano, Oktoba 20, 2010

Ni aibu unakuta mwanamume amevaa amependeza lakini akivua kiatu soksi zimetoboka..

Tazama  picha hiyo ikionyesha soksi ilivyochanika lakini bado inavaliwa vidole vyote nje jamani mbona soksi zipo madukani na ni bei rahisi soksi zipo hadi za shilingi 500 na tena mtu huyu sio kwamba hana pesa ya kununua basi tu sijui ndio anavyopenda.

Tizama upande wa pili wa soksi  au ndio inapitisha hewa,,inawezekana baadhi ya watu huvaa soksi hata kama imechanika kutokana na uvivu wa kununua,au kama ana mke ni uvivu wa mwanamke kutomuandalia vizuri mume wake nguo za kuvaa na kuona ni sawa aende kazini akiwa amevaa soksi iliyotoboka na inapendeza ukiwa na soksi nyingi ili kila siku uwe unabadilisha na kuzifanyia usafi sio unavaa soksi moja hadi inachakaa unaendelea kuvaa.

Kiukweli haipendezi ni vizuri kujitambua na kufahamu nguo zako unazovaa kama imechanika inafaa kushona ishone kama haifai basi jipange kununua nyingine,kwani kwa mtu anayejua kujipenda hawezi kuvaa soksi kama hiyo pichani.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom