Ijumaa, Oktoba 15, 2010

Ukimgundua anayekuibia mpenzi katika mahusiano kama si mvumilivu unaweza ukaua...

Tazama picha hii hawa mabinti wakipigana,matukio kama haya huwa yanatokea pia katika mahusiano.Huko Mkoa wa Lindi wilayani Nachingwea binti Habiba Yusuphu (20)  amelazwa hospitali ya wilaya baada ya kuchomwa kisu na msichana mwenzake mwenye umri wa miaka 18 katika ugomvi unaosababishwa na wivu wa kimapenzi.Inasemekana siku ya tukio Habiba akiwa anasindikizwa na rafiki yake wakitoka katika sherehe ya mahafali ya shule ya msingi Stesheni, alikutana na mtuhumiwa huyo na kuanza kushutumiana kuwa anamchukulia mpenzi wake wa kiume.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi Kamanda wa Polisi mkoani Lindi, amesema inaelekea mtuhumiwa alikuwa amejiandaa kwani wakati mwenzake akiendelea kukataa mara ghafla mtuhumiwa alichomoa kisu na kuanza kumchoma sehemu mbalimbali ya mwili wake mgongoni na kifuani na hatimaye kuishiwa nguvu na kupoteza fahamu.mara baada ya tukio mtuhumiwa alikimbia lakini kwa sasa amekamatwa na yupo kituoni.na Habiba anaendelea vizuri na matibabu.Jamani tutatoana roho kwasababu ya mapenzi na wakati mwingine inawezekana ukachukua uamuzi kwa kitu usichokuwa na uhakika nacho be care friends.


Maoni 3 :

Yasinta Ngonyani alisema ...

mmmhh! kazi kwelikweli mpaka kushikana kabisa kwa sababu ya kupenda. Lakini sasa kuna maana gani ukiitoe roho ya mwenzako.

ADELA KAVISHE alisema ...

asante kipenzi@Yasinta yaani hakuna umuhimu wowowte zaidi ni ujinga tu.huyo wanayemgombania wala hata hana wazo.

o'Wambura Ng'wanambiti! alisema ...

anaiba? ama anaonja na kukuachia?

Jameni kama kingekuwa kiazi ati chaliwa na kuisha ndo ngeshangaa lakini nashangaa zaidi kwa kuwa hupaswi kupigana kwa kitu ambacho hakiliki kikakwisha....lol!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom