Jumanne, Novemba 16, 2010

Jamani kwa nini haya matukio ya ubakaji kila kukicha, Baba ambaka mtoto wake hadi kufa, imetokea sinza Dar es salaam.


Mtoto kama huyu pichani ni mtoto anayehitaji uangalizi wa hali ya juu ili kujiepusha na wabakaji ambapo matukio hayo yamekithiri kila kukicha. Huko Sinza  Mtoto mmoja amefariki Dunia kwa kile kilichodaiwa kuwa kifo chake kimetokana na kubakwa na baba yake mdogo aliyekuwa amelala naye sebuleni tukio hilo ambalo limetokea jana jioni .Imedaiwa mtuhumiwa huyo mwenye umri  wa miaka 19  ambaye naye pia ni mwanafunzi wa shule moja ya sekondari ya jijini alimfanyia unyama huo mtoto wa kaka yake wakati wamelala pamoja sebuleni usiku

Mtoto huyo aligunduliwa na bibi yake ambapo alipigwa na butwaa kumuona mjukuu wake anashindwa kutembea baada ya kumchunguza akagundua kuwa alikuwa ameingiliwa kimwili hivyo akamchukua na kumkimbiza hospitali  ya Sinza Palestina kwa matibabu na baadae kukimbizwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi lakini hata hivyo ilipofika saa 11  jioni alifariki dunia.Maiti imehifadhiwa chumba cha Maiti hospitali ya Mwananyamala na Polisi wanaendelea na uchunguzi zadi limeripoti gazeti la Alasiri jioni leo.Hivii nani wa kumuamini kukaa na mtoto kwani ubakaji umekithiri sio ndugu,,kina baba,kaka na hata jirani kwa nini lakini mambo haya......kweli dunia inaisha


Maoni 3 :

Yasinta Ngonyani alisema ...

Naona ni mwisho wa dunia jamani!!

Bila jina alisema ...

He! jamani sasa watoto wetu tutawaficha wapi?

Mungu tusaidie.

Gg

Bila jina alisema ...

Ama kweli dunia inakwenda mwisho hakuna wakuaminika kabisa tuwaangalie watoto wetu jamani kwa makini sana na tujaribu kuwachukunguza kila turudipo nyumbani kwa wale wanaofanya kazi na kuacha watoto kwa siku nzima.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom