Watoto kama hawa wanakutana na matatizo ya aina mbalimbali likiwemo la ubakaji, matukio ya ubakaji ni matukio ambayo yamekua yakijitokeza mara kwa mara,na watu wanaofanya vitendo hivyo vya kikatili ni watu wazima wakiwemo baadhi ni walimu na wengine viongozi wa dini watu ambao tunawategemea katika kutoa elimu na maadili mazuri kwa watoto na wenyewe kushindwa kustahimili tamaa zao na kuamua kubaka.
Huko mkoani Kilimanjaro Jeshi la Polisi linamsaka Padri Stanslaus Sala wa kanisa Katoliki jimbo la Moshi , parokia ya Mtakatifu Theresa Lego Muro kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa miaka 14 kwa ahadi ya kumpa rozari na mche wa sabuni. Kamanda wa Polisi wa Mkoa Lukas Ng'hoboko, amesema mtoto alifanyiwa uchunguzi katika hospitali ya mkoa ya Mawenzi na kwamba mtuhumiwa ametoroka na anatafutwa.
Akizungumzia tukio mtoto huyo amesema Padri alimchukua na kudai kuwa kuna makosa ameyafanya anastahili adhabu,alidai kuwa waliondoka na Padri kuelekea seminari ya Karumali walipofika Kisanja msituni, Padri alimwamuru ashuke kwenye gari na kumlaza mlango wa mbele na kumwingilia kimwili...Kiukweli tukio hili limenisikitisha sana sijui nani wakumuamini katika malezi ya mtoto niwasikilize wadau..... |
Maoni 3 :
na alaaniwe ka bisa huyo padre!
ni,merudi tena na huku nimeshika nyengo mkononi huyu padre angekuwa karibu yangu leo....we acha tu. Kwanini aliamua kuwa padre kama hawezi kuishi bila kufanya ngono? Na kwa nini kumwingilia mtoto mdogo kiumbe, malaika kabisa. Huu ni unyama kabisa. na sasa anakimbia nini kama anaona si kosa alilofanya. Wanaume hjamani wanaume....
inakera sana wangu sijui hata amekimbilia wapi lakini akipatikana sheria itachukua mkondo wake.
Chapisha Maoni