Jumatatu, Novemba 15, 2010

Mshirikishe Mungu katika kila jambo, kwani familia inayosali pamoja ni familia inayokaa pamoja.

Nimeipenda sana hii picha baba mama pamoja na mtoto wao wakisali pamoja, ni jambo la muhimu sana kila mtu kwa imani yake kutenga muda wa kusali pamoja, kwani hakuna linaloshindikana kwa Mungu katika maisha kuna majaribu mengi yanayojitokeza ambapo tunashauriwa kuwa wavumilivu lakini katika hali ya uvumilivu ni lazima umshirikishe na Mungu ili aweze kukusaidia usikate tamaa. NI JAMBO LA MUHIMU SANA KUMUOMBA MUNGU  TUSIJISAHAU KATIKA HILI.

Maoni 2 :

emu-three alisema ...

Ni jambo muhimu sana kumuomba mungu kwa kila jambo, na kumwamini kwa kweli kuwa yeye ndiye wa kuombwa na hana mshirika

Bila jina alisema ...

wawoo. inapendeza sana jamani. Mungu ndo kila kitu. it seems ni familia bora. me tu napenda kusali sana. Amen

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom