Alhamisi, Novemba 25, 2010

Ukatili wa kutisha shangazi amchoma moto na kumchana viganja mwanawe.Je kwanini baadhi ya wazazi au walezi wanapenda kuwafanyia watoto ukatili??

Mtoto kama huyu pichani ni mtoto ambaye anahitaji kulelewa katika mazingra mazuri lakini mtoto huyu pia kutokana na baadhi ya wazazi na walezi kutokuwa na utu huwatumikisha na kuwanyanyasa watoto.

Mtoto Mariam Abdalah (5) mkazi wa salasala ameokolewa na wananchi baada ya wananchi kuvamia nyumba aliyokuwa akiishi na shangazi yake ambaye alikuwa akimtesa kwa kumchoma mikono na kumchanja viganja  vya mikono. Tukio hilo ambalo limetokea jana saa 4 asubuhi.huko Salasala imedaiwa kuwa mtoto huyo alikuwa akiteswa na shangazi yake  aliyekuwa akimnyima chakula, kumtesa na kumfungia ndani.

Hali hiyo ilikuwa ikiwakera sana majirani na kuamua kumshtaki mama huyo kwa Afisa Maendeleo Julieth Nzugila ambaye aliamua kulivalia njuga suala hilo na kuwashirikisha viongozi wengine ambapo waliamua kwenda moja kwa moja nyumbani kwa shangazi huyo.
Imedaiwa baada ya kufika katika nyumba hiyo walimkuta mtoto huyo akiwa na majeraha ya kuchomwa moto mikononi na kuchanjwa masikioni.Afisa huyo aliamua kutoa taarifa Polisi ambao walifika na kumchukua mtuhumiwa huyo, na mtoto amelazwa Hospital ya Mwananyamala.

Maoni 1 :

emu-three alisema ...

Tujue ubaya hulipwa kwa ubaya...ni swala la muda tu. Ukimtendea mwenzako ubaya, utadhani umeshinda, lakini weka kumbukumbu, sipo siku ubaya wako utalipwa mahala usipotegemea.
Mtese mtoto wa menzako, na wakwako atateswa tu...tumuogope mungu!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom