Jumatatu, Novemba 01, 2010

Uwiano baina ya wapendanao huongeza mvuto..na upendo.

Inapendeza sana kuwa na familia yenye amani na upendo katika picha ni Jadapinket na mume wake Willsmith wakiwa katika hali ya kucheza pamoja, wenza hawa katika historia ya maisha yao wana mambo mengi sana wanayoendana wote ni wanamuziki na pia wasanii wa filamu,,katika maisha tunakutana na watu wa aina mbalimbali na kila mmoja kuna anachokipenda kuna anayependa michezo,kama mpira wa miguu,anayependa muziki na mambo mengine tofauti.Inawezekana wewe una mwenza ambaye hapendi yale unayoyapenda wewe kama ni michezo nk. ikaleta matatizo katika mahusiano yenu.


Ni vizuri kumkubali mwenzio katika hali yoyote na kuheshimu kile anachokipenda,usimkebehi na mara nyingi walio wengi wanatofautiana vile wanavyovipenda.kuna anayependa kilevi mwenza wake hapendi nk.lakini katika hali kama hii ni vizuri heshima ikachukua mkondo wake na utani usizidi kipimo..kwani wengine huishia kuachana na kugombana kutokana na kukosekana na uwiano baina yao.


Maoni 3 :

alice alisema ...

Ni kweli kabisa hayo unayosema ndugu yangu kwani ni vizuri kujaribu kuwa uwiano hata kidogo vinginevyo utakuwa unaumia tu

domina alisema ...

Inawezekana kumpata mtu ambaye mna uwiano lakini isiwe ni katika kila kitu ila kama ulivyosema Adela ni vizuri kuheshimu kile anachokipenda mwenzio na si kuweka dharau

emu-three alisema ...

Upendo wa dhati hutoka moyoni. Nakumbuka siku moja babu yangu aliniambia kuwa utagundua tu huyu ni mke na mume wakiwa barabarani au akiongea na simu.
'Watu wanakua kama wapo katika ugomvi, kuongea kwao kama vile hawataki, na kwenye simu utasikia `ehe, sema, kwani vipi..., lakini awe anaongea na mpenzi wake au nyumba ndogo...mmmh, vipi shosti, vipi mpenze, nimekumiss...'
Kwaweli niliamua kufanya uchunguzi na ukiangalais asilimia kubwa ndivyo ilivyo. Watu wamekaa ndani ya gari kama wanatoka kugombana, akipigiwa simu anakunja uso...jamani hamumuogopi mungu, au hamuitaki pepo...
Sijui, nawaza tu ndugu yangu Adela

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom