Jumapili, Desemba 05, 2010

Hivi ni nini hasa kinachopelekea baadhi ya walimu ambao wanajua maadili mema na mabaya kuwarubuni wanafunzi kwa kuwataka kimapenzi na wengine kubaka????

Nimeyapenda sana hayo maneno kwenye katuni kiukweli haya matukio ya kila kukicha mara  mwalimu kampa mimba mwanafunzi,mwalimu kabaka,mwalimu kafumaniwa na mwanafuzi  na mengineyo ni matukio yakushangaza na kusikitisha  kutokana na kwamba tunategemea mwalimu atamfundisha mwanafunzi maadili mema lakini unakuta mwalimu anabaka au anafumaniwa na mwanafunzi .Hivi nini kinampelekea kufanya hivyo je ni tamaa,ulevi,ulimbukeni au ni nini jamani huwa inauma sana kusikia matukio ya aibu tena yanamuhusisha mwalimu kama kioo cha jamii

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom