Alhamisi, Desemba 02, 2010

Usipokuwa makini unaweza kuvalishwa pete ya uchumba lakini usiolewe.

Inapendeza na huwa ni furaha sana wakati wa hatua kama hii ya kuvishana pete ya uchumba na katika hili wapo walio na nia madhubuti  lakini wengine wakiwa ni matapeli na hivyo kujikuta unaishia kuvaa pete ya uchumba bila ya ndoa na mwisho wake mnatengana na kusahau kabisa kama mlikuwa na malengo ya kuoana.

wapenzi wakifurahi baada ya kuvishana pete ya uchumba kiukweli  inapendeza na ni wengi tunatamani kufanyiwa hivi lakini ni muhimu kujipanga usikurupuke kwani furaha inaweza kuja kuwa kilio

Katika picha hii huyu ni mwanamuziki wa kimarekani Nick akiwa na aliyekuwa mchumba wake wakati wa sherehe yao ya uvishana pete ya uchumba.walikuwa na furaha sana lakini baadae mambo yalibadilika na hivyo Nick kwa sasa akiwa ni mume wa Mariah carely

Hii picha inaonyesha Nick katikati na mikono ya warembo Mariah na aliyekuwa mchumba wake wa zamani na pete alizowavisha baadae alichagua moja na kuamua kujiweka kwa mwanamuziki mwenye sauti tamu ya kumtoa nyoka pangoni Mariah..

Hii ni siku ya Harusi ya  Nick na Mariah. katika hali kama hii kwa wewe ambaye labda ndio ulivishwa pete ya uchumba halafu baadae ukaachwa kwenye mataa na akaolewa mwingine kiukweli inauma sana lakini kama mliachana kwa makubaliano yenu itakuwa ni kitu cha kawaida kwani mapenzi wakati mwingine ni kama safari. MUHIMU KUWA NA MAAMUZI SAHIHI.

Maoni 2 :

Bila jina alisema ...

jamani dada adeladallykavishe.mimi ni mpenzi sana ya glob yako yaani haipiti siku bila kukutembelea sasa niko nje ya mada kidogo naomba unijuze ule wimbo kingereza ulioibwa wakati wamaombolezo ya amina chifupa wa mwanamuziki kutoka marekani alikuwa ni mwanamziki gani?pls naomba mnijuze wapedwa

Bila jina alisema ...

ni kweli wengi wanavisha pete ili tu aendelee kukuchezea, mm ktk hilo niko mjanja mwenzenu inahuu kuvaa pete miaka nenda rudi. tena pete yenyewe akakuvalishie bar, guest, beach nk. wawili tu au na mijamaa na mashost.

kuweni wajanja jamani

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom