Inawezekana ulikuwa na mpenzi wako mlikuwa mnapendana na mliweza kudumu katika mahusiano ya muda mrefu lakini baadaye kutokana na matatizo yaliyojitokeza mwanamume akaamua kuoa mtu tofauti na mwanamke akaolewa na mtu mwingine lakini kibaya zaidi unakuta wengine wanawekeana kinyongo na kuchukiana kitu ambacho nazani kwa upande wangu sio sahihi,,kwani kuna mwingine atatafuta kila njia ili akuharibie maisha na hatopenda ufanikiwe hata siku moja je inawezekana ni kutokana na migogoro iliyokuwa baina ya watu hao au kile kilichopelekea kutengana kwao kinamfanya mmoja kumchukia sana mwenzake maisha yake yote,,,,,,,i need to know more about this jamani..
Maoni 4 :
Labda wivu, na kwasababu kuachana haikuwa tarajio, au kiini cha kuachana , au...yapo mengi na binadamu `chuki' ikijijenga huwa anabadilika hutaamini...ni haya tu kwa leo!
Adela kuna mengi yanasababisha, ila mimi nakupa kutokana na uzoefu ulionipata mimi, wivu na kutokuamini kama kweli naolewa na mwingine na sio yeye, wakati nilipokuwa nae hakuwa ananithamini wala kunijali. wengine wana roho mbaya tu basi anataka akuone unaishi bila furaha.
mara nyingi unakuta wewe ulifikiri ndio umefika lakini mwenzio akakutenda na ukaanza upya na safari + age inakwenda kupata tena chaguu lingine ni kazi basi lazima utamchukia sana hasa kwa sis wanawake
There is a very thin line between LOVE and HATE. Kilichopelekea nyie kuachana ndicho kiletacho chuki. Most of the time aliyeachwa (kuwa dumped) ndie huwa na chuki zaidi kwa mwenzie. Ulikuwa unampenda mwenzio mnashirikiana unaweka malengo yako naye halafu ghafla without any strong anakutafutia kisa anakwambia ' tuachane' au hata hakwambii unakuta mambo yanabadilika, unamfumania...na vitu kama hivyo ukimuuliza anakwambia tuachane. Hata kama una roho ya Yesu utamchukia mtu kama huyu....
Yeye ataona poa tu si ndo amelianzisha.
Chapisha Maoni