Jumatano, Januari 19, 2011

Naomba ushauri nimepata mchumba lakini bado nampenda mpenzi wangu wa zamani nifanyeje..

Habari yako Adela Kavishe samahani kwa usumbufu nilikuwa naomba ushauri kupitia Blog yako
Mimi ni msichana naishi Mlandizi Mkoa wa Pwani ninaishi katika kambi ya Jeshi, mwaka 2010 nilipata mpenzi alikuwa Mzanzibar alikuja kambini kikazi kusema ukweli alinipenda sana kiasi ambacho nilipokuwa nikimtania kuwa  simtaki alilia machozi,hata mimi nilimpenda sana  na wakati tukiwa katika mahusiano   aliwapigia simu hadi wazazi wake kuwa amepata mpenzi.Pia aliniahidi vitu vingi ikiwa ni pamoja na kutoachana  na mimi mpaka mwisho wa maisha yake, lakini penzi halikudumu  sana kwasababu kazini kwao waliamishwa kikazi na yeye akiwa mmoja wapo tena kwakushtukizwa hakupata hata muda wa kuonana na mimi ili aniage.

 kibaya zaidi siku aliyooondoka alikuwa hana simu kwani ilipotea na mimi nilikuwa sina simu kwahiyo mpaka hapo tulishapotezana  katika mawasiliano  na mpaka sasa sijui alihamishiwa wapi ,kinachoniumiza kichwa  ni kwamba kunamtu amejitokeza anataka kunioa na amesema yupo tayari kwa kila kitu  anasubiri jibu kutoka kwangu kwahiyo nilikuwa naomba ushauri kwamba nifanyeje,,,  je nimkubalie huyu anayetaka kunioa au niendelee kuvuta subira  nikimsubiri alyehamishwa .na katika mtazamo wa mapenzi moyo wangu bado unampenda sana yule  aliyehamishwa kikazi kuliko huyu wa sasa...........

Maoni 3 :

Kitomai alisema ...

Waswahili wanasema "Mpende Akupenadye Asiyekupenda Achana Naye! Hiyo ni kauli ya hitimisho kutoka katika waliyoyapitia mapenzi na kuchakachuliwa.Wewe sijui una mtazamo upi katika mambo ya mahusiano. Ni jambo la muhimu, jema na lazima kujiwekea sifa au vigezo juu ya mtu unayehitaji awe karibu na wewe. Hatima ya mambo ya mahusiano ipo mikononi mwako, sisi wengi hatuna uwezo wa kukuchagulia mtu wa kuishi naye zaidi ya kutoa ushauri ambao siyo lazima uufuate.Zaidi unaweza kuangalia move moja ya kinaijeria (jina limenitoka) jinsi ambavyo binti mwenye wachumba watatu alivyochanganyikiwa.

Simon Kitururu alisema ...

Mapenzi ya KUMBUKUMBU nishai hasa kwa kuwa kumbukumbu mara nyingi watu tunazipendezesha !

Mimi naamini kitu halihalisi ya leo kwa kuwa kuna mengi hata niliokuwa nawakumbuka kwa bonge la uzuri nilipojitahidi kukutananao tena baada ya miaka nikagundua kuwa mengi yalipambwa na kumbukumbu na wala sio hali halihalisi.

Nachofikiri ni kuwa huyu mpenzi wako wa sasa kuna kitu unawasiwasi nacho na kumbukumbu za mchumba wako wa zamani ni kama Kinga na sababu ya kukufanya uwe na sababu kwanini huingii kichwakichwa.

Ila mimi nafikiri ni afadhali umchukue huyu wa sasa kuliko yule wa kumbukumbu au achana nao wote subiria mwingine kabisa!

Ni mtazamo tu!:-(

happy alisema ...

mi naoana ifike mahali uangalie nn kina usika.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom