Matukio ya mimba za utotoni yamekua yakikithiri kila kukicha,Huko mkoani Mbeya binti mwenye umri wa mika 9 ambaye alikuwa akiishi na mama yeke mkubwa baada ya mama yake mzazi kufariki,,amejifungua mtoto inasemekana alipewa mimba na kaka yake ambaye ni mtoto wa mama yake mkubwa mwenye umri wa miaka 18, na alipobainika kuwa ni mjamzito alifungiwa ndani na mama yake huyo ili wananchi wasibaini tukio hilo. Mtoto huyo amesema kaka yake alikuwa akimtishia kwa kisu na kumlazimisha kufanya kufanya naye ngono jambo ambalo anadai lilimfanya akubaliane naye, aliongeza kuwa anamshukuru Mungu kwa kujifungua salama mtoto wa kike lakini mama yake huyo alishindwa kumpa huduma nzuri hivyo kupata vidonda sehemu za siri vilivyosababisha kutokwa usaa mara kwa mara,,cha kushangaza mama huyo hakuwahi kuonyesha dalili za kumpeleka binti huyo hospitali, baada ya polisi kupata taarifa hizo walimlazimisha kumpeleka hospitali na baada ya kufika huko alidanganya umri akidai kuwa ana miaka 14 huku akisisitiza umri huo....jamani imenisikitisha sana hili ni tukio la kikatili........ |
Maoni 1 :
Sheria ingechukua tu mkondo wake, kwani mtoto akizaliwa wanaweza kuthibitisha madai yake kwa njia ya DNA test. We sema tu mnyonge hana haki!
Chapisha Maoni