Alhamisi, Februari 10, 2011

Je ni lazima kwa yule asiye na mpenzi kutafuta mpenzi katika siku ya Valentine?

Jamani ni kweli inapendeza kuwa karibu na kufurahi pamoja na umpendaye katika sikukuu ya wapendanao lakini kwa yule ambaye hana mpenzi siyo lazima atafute mpenzi kwa siku hiyo,

Baadhi ya watu wanaichukulia siku hii vibaya kwa kuona kuwa ni siku ya kufanya ngono,, wengine unakuta ni waume za watu badala ya kusherekea sikukuu hii na wake zao wanaenda kutafuta wanawake nje haipendezi kufanya hivyo kwani katika sikukuu hii ni vizuri kusherekea na familia yako au na yule umpendaye na si vinginevyo

Furahia sikukuu ya wapendanao hata ukiwa hauna mpenzi kuwa karibu na ndugu jamaa na marafiki.

Maoni 2 :

Bila jina alisema ...

Ni kweli kabisa na pia ni vema tukikumbushana kuwa siku hiyo moja tusipokuwa makini badala ya kusherehekea matokeo yake tunasherekea kwa kuambukizana magojwa yasiyokuwa na tiba kama Ukimwi, ni vema kila mtu akawa makini na kile atakachokiona ni furaha kwake.

Hashir alisema ...

mambozzz Ade? Long time no chat, hope you good wangu!! kwa upande wangu mimi naona hili halina haja, coz mchumba hatafutwi kwenye sherehe hehee unaweza ukachagua asiye stahili, ila basi tu mambozz ya poudaah! Ila kimtazamo wa kawaida, kama kweli hauna mchumba na umempenda basi jaribu bahati yako! But hii siku sio vizuri kuitumia kwa kumsaliti mwenzio aliye mbali na wewe....bye nisalimie fb! mimi labda mwezi wa sita ndio nitarudi fb lol..take care!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom