Ijumaa, Februari 25, 2011

kulalamika katika mapenzi kuna jenga au kuna bomoa????

Inawezekana hali ya kulalamika ikatokea katika mahusiano ikiwa ni  kutokana na matatizo yaliyojitokeza katika mahusiano mliyonayo, kwa mfano kama mwanamke au mwanamume amekuwa akifanya makosa mbalimbali ambayo uridhishwi nayo kama ulevi,matumizi mabaya ya pesa,usaliti nk na hivyo kupelekea malalamiko ya hapa na pale, na katika hili wanaoongoza kwa kulalamika ni wanawake kiukweli hali ya kulalamika huwa inajitokeza lakini ni bora kutafuta njia nyingine ya kutatua matatizo kuliko kukaa ukilalamika kuwa unaonewa inawezekana wewe ndiye chanzo lakini ukawa unamlalamikia mwenzio kila kukicha.MUHIMU KUKAA CHINI KUTAFAKARI TATIZO LIMEANZIA WAPI NA SI KULALAMIKA,,wakati mwingine kuna walio na tabia ya kulalamika bila sababu yaani ndivyo alivyo na hiyo hupelekea baadhi ya wanaume kuchelewa kurudi nyumbani kwasababu anajua akifika nyumbani kila kukicha mke wake haishi kulalamika bila sababu tumia njia nzuri,,usikurupuke tulia ili uweze kutatua tatizo.

Maoni 3 :

Hashir alisema ...

Salaaam Ade, hope mzima wa Afya! Hili suala la kulalamika kwa kweli sio zuri hatakidogo, kama mwenzio amekuudhi kwa jambo fulani ambalo labda kalifanya kinyume na matashi yako, basi muite pembeni au msubiri ndani pekeyenu, halafu tafuta njia ya kumueleza taratibu kama vile unamshauri jambo, nakama mtu mwenye akili basi atafahamu tu. Ukianza malalamiko yakila siku lazima utakuwa unamboa mwenzio na itafika time as you said kwamba hata kurudi nyumbani anaona kama kituo cha polisi, yaani kutwa malalamiko na maswali juu yake. Haifai sana kulalama lalama kila wakati katika mahusiano.....Mapenzi ni raha sio karaha! Thanks.

Simon Kitururu alisema ...

Kulalamika kunaweza kujenga ingawa kunaweza kubomoa ukiniuliza mie!:-(

Na naamini kulalamika huwa kuna sababu ingawa kulalamika kunaweza kuwa chanzo chake sio kile kinacho lalamikiwa!:-(


kipengele hiki:``...inawezekana wewe ndiye chanzo lakini ukawa unamlalamikia mwenzio kila kukicha.MUHIMU KUKAA CHINI KUTAFAKARI TATIZO LIMEANZIA WAPI NA SI KULALAMIKA´´´-mwisho wa nukuu!

Nakifagilia sana!

Lutonja Fita alisema ...

Adela ujumbe wako mzuri umenigusa hata mimi mwanasaikolojia kwani kwa mujibu wa mwanasaikolojia mwenzangu wa chuo kikuu cah DODOMA Dr. Kisanga au Madamu Dr. Kisanga aliwahi kunena ya kwamba ndoa nyingi zinavunjia kwa sababu ya wanawake kupenda pesa na kila siku kuwalalamikia waume zao kwa kuwaambia matizo chungu nzima.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom