Jamani katika mapenzi mambo mengi sana yanaleta migogoro katika mahusiano nimepata ujumbe huu kutoka kwa Suzi anaomba ushauri "mimi ninaye mpenzi tumekuwa katika mahusiano kwa miaka miwili sasa tatizo ni kwamba amekuwa na tabia ya tofauti tokea nilipomtambulisha kwa marafiki zangu kila siku ananiambia marafiki zako ni wazuri sana wanajua kupendeza na wanaenda na wakati tena kuona hilo halitoshi huwa ananiambia hivyo hata mbele ya marafiki zangu, naumia sana moyoni kwani nahisi hanipendi na yeye anataka na mimi niwe kama marafiki zangu sasa sijui nifanyeje, hivi huyu mtu ananipenda kweli au naombeni ushauri |
Maoni 3 :
Achana nae huyo anatamaa c kuwacfia tu wakikaa sawa anakula mzigo.nawajua tabia zao c watu wa kuaminika ki hivyo.take care.kama anapenda wanavyo vaa c akununulie na wewe uvae kama wao.mwambie atoe pesa nawe upendeze.
Muelleze hilo tatizo kuwa anakuumiza na kama akiendelea basi anakuumiza makusudi na hakupendi kisawasawa. Na kama tujuavyo wengi hawastukii kitu safi wakati wanacho na hutamani vya wengine mpaka wapoteze vyao ndio hustukia .Nasema hivyo kwa kuwa kutokana na lalamiko lako naamini umempenda sana huyo jamaa na labda huko atamaniko hawezi pata kama wewe na ndilo litakalo kuwa juto lake mbeleni kama ataendekeza kutamani kwa staili ya : The grass is always greener on the other side of the fence .
I never thought I would agree with this option.
Chapisha Maoni