Mawasiliano ni nguzo kuu katika mahusiano ikiimarishwa huchochea amani ya kudumu lakini ispozingatiwa basi husababisha matatizo baina ya wapenzi na hata kupelekea kuachana,mawasiliano baina ya wapendanao yapo katika njia mbalimbali ikiwemo katika simu ya mkononi, kwa kuzungumza mkiwa pamoja nk, na katika hilo ni vizuri kujifunza lugha inayoweza kukufanya uelewane na mwenzako, ukizingatia sauti yako unayozungumza ukiwa mtaani iwe tofauti ukiwa na mwenza wako chumbani,mfano huwa una tabia ya kuzungumza na wenzako kwa lugha za mkato kama wewe,nipe,toka nk mwenzi wako hutakiwi kuzungumza naye katika lugha hizo, Kuna Lugha ya kuzungumza ukiwa na mwenzi wako ni mwiko kutoa sauti ya kuamrisha ni vizuri kumnyenyekea lakini si katika kiwango ambacho kitakufanya uonekane una kasoro za kisaikolojia,, kinachotakiwa ni kuweka mbele hisia zako, pia upole uliopitiliza hauna maana kwamba wewe ni mpenzi sahihi, ni vizuri kujitambua na kujiamini |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni