Jumatatu, Machi 28, 2011

"Ninayempenda hanipendi nisiyempenda ananipenda niende kwa nani "naombeni ushauri

Habari yako Adela pole na majukumu mimi naitwa Michael naishi Morogoro  kuna tatizo linalonisumbua katika mahusiano, ni kwamba kuna msichana nimetokea kumpenda sana lakini yeye hanipendi na hataki hata kuniona lakini mimi moyo wangu unampenda sana na wakati huo huo kuna dada mwingine ambaye yeye amenitamkia kuwa ananipenda sana lakini mimi simpendi kwasababu nampenda mtu mwingine yaani simpendi hata kidogo ijapokuwa yeye anajitahidi kunionyesha mapenzi ya kila aina,,mimi nia yangu niwe na yule ninayempenda lakini yeye hanitaki sijui nifanyeje naombeni ushauri kupitia Blog ya Adela,,,haya ni mambo yanayotokea katika mapenzi unayempenda hakupendi,,usiyempenda anakupenda nini cha kufanya katika hili

Maoni 4 :

Rik Kilasi alisema ...

Mimi ninavyo jua mapenzi haya lazimishwi so kama mdada hakupendi jipange upya utapata anaye kupenda.Kwasasa ni vema kuwa bize na mambo yako bila kusahau kumuomba Mungu akupe mke mwema.Si kila anaye kutamkia anakupenda ni mkweli ila wapo wa kweli kama upo siriaz anaye kupenda utamjua tu.Bila shaka hata huyo unayesema hakupendi ni huenda hana uhakika kama kweli una mpenda so lazima ajue kama kweli unampenda pengine hata approach yako kwake inampa wasiwasi kua ( ni wale wale wapita njia)

Pamoja na kusema hayo yote akili ya kuambiwa changanya na yako bila kusahau kumshirikisha Mungu with time utapata waukweli ambaye ndio mke mwema.Kila lakheri bro

Bila jina alisema ...

Hiyo ni njia panda kwakweli. Mi nakutana na hili tatizo sasa. Nina rafiki wa kiume ambaye kiukweli ni my dream man lakini jamaa ananipelekesha sijaona... yaani sijui nijielezeje mnielewe hana mpango kabisa na mimi pale tu anapokuwa amezidiwa na anataka cha hap chap ndo atanikumbuka lakini nampenda hamna maelezo. Kuna kaka mwingine yeye kwa kweli ananipenda mno, mpaka namuonea huruma, mi yaani hata kumuona sitaki... ahta sielewi nifanyeje, jamaa ananiabuse na nashindwa kumuacha, na huyu ananipenda mno lakini misimpendi.....!!!

Bila jina alisema ...

Kwa kweli hii inachanganya sana. Nawaomba ushauri na mimi nielekee wapi.Nimeolewa tumetengana. Nina mpenzi (mume wa mtu )Ananipenda sana, na hubeba shida zangu kuliko hata za kwake. Mimi ndiyo kabisa hata mshipa haushtuki kwake. Halafu nina kijana hajaoa ananipenda sana na mimi nimekufa kwake. Huduma ya yule mume wa mtu naitaka ila sina mapenzi naye, na mapenzi ya huyu kijana yako juu sana , ila huduma nyingine hakuna. Nizingatie wapi? ? ?
Msinirudishe kwa mume tumetengana kabisa.

Unknown alisema ...

Hi waungwana!!, matatizo ya kimapenzi hayaishi hapa Duniani, suala la msingi ni uvumilivu na kujiamini, kama mtu hakupendi achana naye angalia mbele, kwani kama hakupendi utakaa kupoteza mda wako bule huku ukijua hupendwi. Raha ya Mapenzi upate UNAYEMPENDA NA ANAKUPENDA KWA DHATI.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom