Jamani nimepata ujumbe huu kutoka kwa James, "Mambo vipi Adela pole na majukumu mimi ni mwanaume mkazi wa Arusha nina mpenzi wangu nilikuwa nampenda sana na wakati tunaanza mahusiano alikuwa ni binti mrembo na mwenye rangi nyeusi ya kuvutia,katika mahusiano yetu tuna takribani miaka miwili na nilikuwa na lengo lakuja kumuoa hadi kwao nilishajitambulisha sasa kilichokuja kunishangaza ni baada ya mpenzi wangu kwenda Dar es salaam kusoma ambapo baada ya miezi mitatu amerudi ni mweupe kama mzungu na alikuwa mweusi kiukweli hii hali imenichukiza sana na hata yeye nikimuuliza kwa nini ameamua kujichubua anasema anapenda kuwa mweupe kutaokana na alichokifanya mimi nahisi kupunguza mapenzi kwake lakini yeye anaonyesha kunipenda sana kiukweli rangi aliyonayo sasa siipendi na kila kukicha anazidi kuwa mweupe kwa kujichubua na hataki kuacha. NAOMBENI USHAURI KUPITIA BLOG YA ADELA. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni