Jamani usipokuwa makini sikukuu ya wajinga ambayo huazimishwa kila mwaka tarehe moja mwezi wa nne inaweza kuleta migogoro kwa wapendanao,,, kwasababu kuna baadhi ya wapenzi siku ya leo wamegombana kutokana na kudanganyana kuna vitu kama kumtumia ujumbe mpenzi wako nakumuambia kuwa mimi sikupendi kuanzia leo tuachane huku ukiwa umefanya hivyo ukijua kuwa unamdnganya kuwa ni sikukuu ya wajinga kuna dada mmoja amemfanyia hivyo mpenzi wake halafu baada ya muda alipoona mpenzi wake amemjibu kuwa ;;kama umeamua tuachane mimi sina kipingamizi basi wewe endelea na maisha yako,,alipojibiwa hivyo alichanganyikiwa na kumpigia simu mpenzi wake huku akimwambia nilikudanganya jamani si unajua ni sikukuu ya wajinga yule mwanamume alikasirika na kumwambia kama umeniona mimi ni mjinga basi na mimi nitabaki na ujinga wangu sikutaki tena,,,haya jamani hadi muda huu huyo dada analia anajuta kumdanganya mpenzi wake,,,sasa sijui wewe unaonaje hili....wengi hutumia kudanganya katika sehemu tofauti wengine hudiriki kusema kuwa amekufa ili kumshtua mpenzi na mambo mengine,, inakubidi uwe makini pale unapomdanganya mwenzio hakikisha yupo katika hali nzuri na awe ni muelewa vinginevyo inazuwa mtafaruku...... |
Maoni 1 :
kwakweli huyo jamaa naona ndo alipopatia chance since hiyo haiwezi kua sababu ya kumuacha mtu unaempenda dearly.
Chapisha Maoni