Jumatano, Aprili 13, 2011

Tumia matunda aina ya parachichi (avocado) na upate faida zake.

 Tunda hili lina kiasi kidogo cha maji tofauti na matunda mengine tuliyozoea kula.

 avocado lina kiwango kikubwa cha mafuta na ndani ya kiasi hicho cha mafuta kuna tindikali (acid) mbalimbali zinazosaidia kukinga na kutibu maradhi katika mwili.

 tunda hili pia lina kiwango cha juu cha protini kutegemeana na aina ya tunda lenyewe. Ndani ya protini pia kuna tindikali (acid) aina ya amino.

: inadaiwa kuwa tunda hili lina kiwango kikubwa cha vitamini E kuliko ile inayopatikana kutoka kwenye mazao ya wanyama, hata mayai hayana kiwango kikubwa ukilinganisha na tunda la avocado.

VITAMINI "B6": Nayo inapatikana kwa wingi.

MADINI YA CHUMA (Iron): Pia yapo kwa wingi.
 
 

Faida zinazotokana ama kwa kula au kutumia tunda la avocado au matumizi ya mmea wenyewe. Kwanza kabisa ningependa ujue kwamba majani ya mti wa avocado pamoja na magamba ya mti wake yakitengenezwa vizuri yanatumika kutibu maradhi ya kuharisha, kuondoa gesi tumboni, kutuliza kikohozi pamoja na matatizo ya ini na kusafisha njia ya mkojo. Dawa hii haishauriwi kutumiwa na akina mama wajawazito kwani inaweza kuwaletea matatizo yanayoweza kuharibu mimba. Aidha kwa wanawake ambao wameshindwa kuona siku zao kwa wakati, wanaweza kutumia mchanganyiko huo kwa nia njema ya kuwawezesha kuingia kwenye period.
 
 
 


Tunda la avocado ni chakula kizuri kwa watoto, pia lina madini ya potasiam (potassium) na vitamin B6 na E ambazo zinaweza kuleta nafuu kwa wale wenye matatizo ya stress, matatizo ya uzazi kama ugumba na uanithi. Tindikali aina ya oleic (oleic acid) iliyomo ndani ya tunda hili inasaidia kukinga dhidi ya magonjwa ya moyo, kiharusi na kansa. Aidha tunda hili linasaidia uyeyushaji wa chakula tumboni hasa kwa wale wenye matatizo ya vidonda vya tumbo, kwani tunda hili lina "fiber" ambayo ni muhimu kukinga kuta za utumbo. Watu wenye maradhi ya anaemia, diabetes, matatizo ya mfumo wa neva, matatizo ya artery wanashauriwa kula tunda hili mara kwa mara. Tunda la avocado limethibitishwa kupunguza kwa kiwango kikubwa cholesterol kutoka kwenye damu hasa kwa wale wenzangu na mimi ambao ni wanene. 
 
 


Matumizi ya nje ya mwili kwa tunda hili husaidia kulainisha ngozi na kuondoa makwinyanzi, kung`arisha na kulainisha nywele na kuzifanya zionekane nadhifu, linasaidia ukuaji wa nywele na pia kuimarisha na kuzuia kukatika kwa nywele.

Maoni 6 :

Bila jina alisema ...

asante sana kwa mada nzuri ya kutuelimisha, ila naomba kujua hayo majani ya mti wa avocado pamoja na magamba ya mti wake yantengenezwaje hadi mtu aweze kuyatumia kama dawa? Tina!

Yasinta Ngonyani alisema ...

Ahsante Adela kwa somo hili nzuri!!

ADELA KAVISHE alisema ...

mdau hapo juu majani na magamba unachemsha na maji hadi ichemke vizuri kisha unaacha inapoa vizuri unakunywa katika kikombe angalau mara moja kila baada ya siku mbili ndani ya wiki utaanza kuona mabadiliko,vinginevyo jaribu kuwaona wataalamu kwa msaada zaidi

Unknown alisema ...

Hadi hamasa.

Mwanawakwe Nanyika. alisema ...

Jamani nimefurahi sana,mimi nina tatizo la kupata damu ya hedhi,na nimesgahangaika sana kutafuta mtoto wa pili kwa muda wa miaka 7 sasa,hapa njee kwangu kuna mparachichi,naanza jioni ya leo kuuchemsha,asante sana dada Adela.

Bila jina alisema ...

Thank you cster

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom