Alhamisi, Mei 19, 2011

kama mwenza wako zamani alikuwa na wivu sana lakini siku hizi wivu umepungua kabisa kuna umuhimu wa kukaa na kutafakari mabadiliko hayo

Katika mahusiano mwanzoni inawezakana mwenza wako alikuwa ni mtu mwenye wivu sana akipenda kufuatilia kila unachokifanya kwa mfano akikupigia simu  anataka upokee haraka bila kuchelewa vinginevyo inatokea ugomvi, alikuwa ni mtu ambaye anapenda sana kukagua simu yako na kutaka kufahamu nani amekupigia na namba za simu zilizomo pia kufahamu kila utakapokuwa na nini unafanya kwa wakati huo, nk. inawezekana hali hii ilikuwa inakukera sana kutokana na kwamba ulikuwa hupendi kufuatiliwa kwa kiasi hicho na mara nyingi kujikuta mkigombana na mwenza wako.

Lakini baada ya muda mambo yanaanza kubadilika na yule mwenza wako anapunguza ghafla kukufuatilia yaani inakuwa tofauti na ulivyozoea  kuwa nikifanya jambo fulani mwenzangu anakuwa mkali  lakini unashangaa ukifanya hilo jambo hana muda hata wa kukuuliza na katika hali hii inawezekana mwenzako ameamua kukupa nafasi baada ya kuchoka kukufuatilia, au ameanzisha mahusiano mengine hivyo anakuwa hana muda na wewe, na inapotokea hali hii inabidi ukae na kutafari mbona zamani mpenzi wangu alikuwa na wivu  sana? lakini siku hizi wivu umepungua je nini kimesababisha haya mabadiliko? inabidi ukae chini na kutafakari ili kupata jibu sahihi kwani inawezekana mabadiliko ya ghafla yakawa na jambo ambalo limejificha ndani yake.

Maoni 3 :

Bila jina alisema ...

Lakini kumbuka kuwa wivu ni uoga na kutojiamini. Mwanamme au mwanamke mwenye wivu anauoga fulani ndio maana anaweka wivu kwenye relationship yake ili aweza kuficha mambo mengine...mtu mwenye wivu hajiamini pia ...sasa kama wivu ukiisha sio kuwa kuna jambo ila ni kuwa amejiamini katika ile relationship na ameweka 110% hivyo hana wasiwasi tena..

emu-three alisema ...

Wanasema wakati mwingine ukimchunguza sana samaki utashindwa kumla...mmmh ni kweli huenda kuna jambo, lakini pia inawezekana ikawa sababu ya juhudi zako mwenyewe kumweka sawa. Tukumbuke wanadnoa au wapenzi ndio wanaoweza kujenga au kubomoa ndoa yao!

Simon Kitururu alisema ...

Naamini hakuna mtu yoyote mwenye simu hata ambaye hana mtu mwingine kipenzi awezaye kufanya ya mwanzo daima!

Na kama uko na mtu akupendaye na alivyokuwa anakupigia simu mwanzoni na baada ya miaka kumi bado anafanya hivyohivyo! Mchunguze kwa kuwa anakasoro huyo!

Haki ya nani kama unampenda mpenzi wako na unatabia ileile mbele yake hata baada ya mwaka baada ya kujua ni wako huyo!
Labda unakasoro wewe au anakasoro yeye!

Na kuchokana kwa kawaida KIBINADAMU inasemekana ndio KAWAIDA!:-(

Ni mtazamo tu huu na wala sio neno la BIBLIA!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom