Jumapili, Mei 08, 2011

Majina kama mpenzi,sweety,,honey au baby yanaongeza mvuto katika mapenzi


Katika mapenzi majina ya kimapenzi yana mvuto sana inapendeza kukuta unamuita mpenzi,mke au mume wako majina kama honey,baby,sweety,darling nk. kwani majina haya huongeza mvuto zaidi katika mahusiano mliyonayo ni wazi kuwa baadhi ya walio wengu huitana majina yao binafsi na kuna wengine unakuta mwanzoni mwa mahusiano majina haya ya kimapenzi yanatawala sana lakini baada ya kuzoena wanaitana majina yao na wengine hudiriki kuitana majina kama wewe, utafikiri hamjui anayemuita.

kiukweli majina haya ni mazuri sana kuyatumia katika mahusiano kwani unaonyesha hisia zako juu ya yule umpendaye bila kificho na hili ni kwa wote iwe mwanamume au mwanamke kwani tukiangalia kwa asilimia kubwa wanawake ndiyo wanapenda kutumia majina haya kuliko wanaume na wengine hawapendi kutumia majina haya kwa kusema kwamba ni "uwizi mtupu" kutumia majina haya ya kimapenzi. lakini kumbuka majina ya kimapenzi ni chachandu moja wapo katika kuongeza ladha ya penzi.


Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom