Jumanne, Mei 31, 2011

Nini kinapelekea baadhi ya wanaume kuwasaliti wenza wao pindi wanapokuwa katika hali ya ujauzito??

Ni wazi kabisa kwa asilimia kubwa baadhi ya wanaume huwasaliti wenza wao pindi wanapopata ujauzito, leo nilikuwa nazungumza na mama mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe amenisimulia namna ambavyo mume wake aliweza kumsaliti kipindi akiwa mjamzito tena huku akimuonyesha wazi amesema "kiukweli wanawake tunakutana na matatizo mengi sana katika ndoa mimi mume wangu kipindi nikiwa mjamzito alianza kunifanyia vituko vya kila aina mwanzoni mimba ikiwa na miezi mitatu hadi mitano kidogo ilikuwa afadhali anarudi nyumbani mapema tunalala pamoja.

lakini ilipofika miezi sita na kuendelea mambo yalibadilika akawa analala nje akirudi amelewa nikimuuliza kwa nini ananifanyia hivyo ananijibu kuwa ni muda wake wa kufurahi  kwani mimi siwezi kumridhisha kwa lolote kutokana na hali niliyonayo, nilitamani kuondoka lakini ndugu zangu walinishauri nivumilie,nilipata mateso kwa muda mrefu hadi nilipojifungua ndipo tabia yake ilianza kubadilika  alianza kuwahi kurudi nyumbani huku akiniomba msamaha kwa yaliyotokea, nimemsamehe lakini  wakati mwingine huwa najiuliza je nikibeba tena ujauzito atarudia tabia yake ya zamani?? "Nawashauri akina baba wawe na roho ya huruma kipindi mama akiwa mjamzito ndiyo anahitaji msaada wako zaidi.

Maoni 9 :

Bila jina alisema ...

ni tamaa tu ya baadi ya wanaume hakuna kingine,pole sana mama kwa yaliyokukuta ila kuwa makini na huyo mume wako

Bila jina alisema ...

jamani wanaume wenye tabia kama hii embu wajaribu kufikiria kama ingelikuwa ni yeye anafanyiwa hivyo angejisikiaje,, tupendane katika shida na raha

Bila jina alisema ...

unajua nini Adela wanawake wakiwa wajawazito wana matatizo sana unakuta mwingine mimba inampelekea kumchukia sana mume wake sasa hali kama hiyo inamfanya mwanamume kutafuta faraja sehemu nyingine

emu-three alisema ...

Lakini mimi najiuliza nini matokeo ya `pendo'...nikiwa na maana unapopanda mbegu shambani unategemea nini, au `ndio kisasa' kuwa kulitakiwa kujilinda...!
Jamani watoto (mimba) ndio matokea ya tendo, sijui la ndoa au la mapenzi, ukikataa mtoto wewe huna tofauti na muuaji! Kwasababu gani huyo mama anaweza kuamua kuitoa hiyo mimba, au akamtupa huyoo mtoto...nani kasababisha haya kama sio wewe!
Kama hatutaki mimba, tuache tendo lenyewe!

Bila jina alisema ...

FARAJA GANI BANA WEE NDO SHIDA NA RAHA HIZO WANATAKIWA KUVUMILIA KIPINDI CHA MPITO HICHO JAMANI UNATAKIWA WW NDO UMTIE FARAJA MWENZIO HIVI MNAJUA NI EASY TASK HIYO EEH.LAITI NANYIE MNGEKUWA MNABEBA MIMBA MNGEKUWA NA MAPENZI JAMANI MANA MTU MWINGINE HUJUA MACHUNGU YA KITU FULANI BAADA YA KUKIPITIA NA YY INGAWA CYO FORMULA MANA KUNA BINADAMU WANA ROHO NGUMU HATARI.SO ALL AND ALL TUVUMILIANE KIPINDI CHA MPITO HIKI JAMAN KHAA.

Bila jina alisema ...

mi nawaambia mtu usipokuwa makini unaweza kujikuta unaachana na mke wako kipindi cha ujauzito hususani kama mimba yake imempelekea kukuchukia wewe cha muhimu ni kuwa wavumilivu tu

Bila jina alisema ...

mimi naona ni tamaa tu inawezekana kumvumilia kipindi cha ujauzito basi tu baadhi ya wanaume wanajifanya hawawezi

Bila jina alisema ...

Hivi mbona hata kula tunakula hotelini?Kwa nini tusirudi nyumbani kula kama tuna njaa?Mimi najua tu kwamba kula hotelini hakumaanishi nimehama nyumbani bali natuliza ule mzuka wa njaa kwa wakati ule tu, lakini lishe yangu makini bado ni ileile ya home.

Kwa hiyo kula nje ni kutuliza ghasia za mihemko,lakini mlo kamili upo nyumbani. Kuna kujifurahisha kidogo na radha nyingine unapopata nafasi na hilo haliondoi unyumba ulio nao bali linasaidia kutuliza dhoruba inayovuma kwa sekunde chache.

Mambo ya ndoa yasikie tu bombani, maana wengi mnashupalia tu kusema ooh unasaliti pasipo kuingia kwa kina na mapana na marefu.Mimi mwanaume nakula nje kwa ustaarabu ili kupata mapenzi,lakini ndoa inatunzwa vema.

Suala si wakati wa uja uzito tu bali nyakati zote zina kashikashi za hapa na pale ambazo zinahitaji huduma ya nje kidogo ili kunusuru ndoa mradi tu unazingatia eneo la ndoa na majukumu.Chakula cha hotelini unabembelezwa na kuhudumiwa vizuri mno japo ni kwa dakika chache tu unakuwa pale.Home ndipo pa kutua mzuka mzima wakati tayari umepooza mahali.

Bila jina alisema ...

Wnaume wengi hajishughulishi na kupata elimu inayohusu wakinamama na tabiaa zao hususani wakati wakiwa wajawazito. nasshauri wanaume tujielimishe ali tuweze kukaa kwa uvumilivu na uaminifu katika kipindi kama hicho.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom