Jumatano, Mei 11, 2011

Tumia juisi ya kuandaa mwenyewe ili kupata virutubisho asilia, jinsi ya kuandaa Juisi ya tikiti maji na embe

Mahitaji ya kutengeneza kinywaji hiki ni pamoja na tikitimaji moja, embe moja,tangawizi kijiko kimoja,ndimu moja, sukari robo kikombe cha chai.Baada ya kuwa na mahitaji haya tunakuja kwenye NAMNA YA KUANDAA,, Menya tikitimaji na likate vipande vidogovidogo kisha weka kwenye mashine ya kusagia, menya embe kisha katakata na kisha tumbukiza katika mashine ya kusagia kama ulivyofanya kwenye tikitimaji, baada ya kuchanganya pamoja kisha tia ndimu iliyokatwa vipande kiasi pamoja na maganda yake na tangawizi pia, kisha baada ya hapo weka sukari, anza kusaga mpaka uhakikishe mchanganyiko umelainika vizuri.

Baada ya kuona mchanganyiko wako umelainika miminia kwenye jagi  tayari kwa kunywewa, pichani ni muonekano wa juisi ya tikitimaji na embe.

Juisi ya kuandaa mwenyewe ni nzuri zaidi na unaweza kunywa juisi wakati wowote ikiwa asubuhi mchana, au jioni ikiwa ni baada ya kula au kabla ya kula chakula.

Maoni 4 :

emu-three alisema ...

Nimekuta mate yananitoka, shukurani kwa utaalamu huo

Simon Kitururu alisema ...

Duh ngojea nikatafute matunda!

Unknown alisema ...

HII safI

Unknown alisema ...

HII safI

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom