Jumatano, Juni 29, 2011

Je!Inawezekana ukaishi na mwenza wako kwa muda mrefu lakini hata siku moja hajawahi kukuambia neno nakupenda mpenzi au maneno matamu ya kimapenzi.?

Katika mahusiano inawezekana kuna baadhi ya wapenzi unakuta mwanzoni wa uhusiano neno nakupenda, nakuhitaji na maneno mengine matamu katika mahusiano  huwa yanachukua nafasi kubwa sana mwanzoni lakini baadaye ikiwa ni kwenye ndoa au mahusiano ya muda mrefu maneno haya yanaanza kupotea chanzo kikiwa ni mazoea na mbali na mazoea pia yawezekana kukosekana kwa ubunifu pamoja na mwanamume au mwanamke kuwa na mahusiano nje hivyo kupelekea kupunguza mapenzi kwa mwenza wake nakumuona kama ni kero kwake.

  Ni wengi walio katika mahusiano unakuta wanaishi alimradi maisha yaendelee lakini uhusiaono walionao una matatizo makubwa jambo la muhimu ni kuzungumza kabla haijawa hatari kwani kama unaona kuna mapungufu yoyote katika mahusiano uliyonayo ni bora kuzungumza na mwenzio ili muweze kutatua matatizo yenu mapema kumbuka maneno matamu katika mapenzi huongeza chachu katika mahusiano.

Maoni 5 :

o'Wambura Ng'wanambiti! alisema ...

ukiliangalia kwa mtizamo wa kisasa unaweza kuona kama hakupendi ila ukiliangalia kwa mtizamo wa kizamani ni kawaida tu...si lazima aseme 'sweetie, honey, darling nk' ndo ujue anakupenda.

ni mtizamo tu!1

Hashir alisema ...

Yaani dally, we acha tu. Mambo kama haya yapo tena sana katika jamii zetu, utakuta mtu anaishi na mwenziwe katika mahusino kwa uzuri sana, lakini baada ya muda mkubwa kupita, utakuta haya maneno mazuri hayapo kabisa, wanaona wenyewe wanaishi, lakini kumbe raha ndani ya mahusiano inapotea!! thanks sana kwa ukumbusho wako...

Simon Kitururu alisema ...

Ila inasemekana asilimia kubwa ya maneno matamu ni uongo!:-(

emu-three alisema ...

Maneno ya kimapenzi ni kama kachumari katika mapenzi...ni kama mtu angekuuliza hivi unaweza kula pilaubila kachumbari...jibu ni ndio,lakini kwanini tusilienzi penzi letu likawa linashamiri kila siku...sababu kubwa ni kuwa tunachukulia kuwa mkishaoana basi tena, nyie ni kama `kaka na dada'...haiwezi ikawa hivyo ila nachukulia mfano!
Wanandoa, tukumbuke kuwa ndoa ni nusu ya `imani'...ya kwamba ukiiboresha ndoa yako na mkawa na amani na upendo ni kuwa nusu ya imani yako kwa dini yako umeipata vyema na ni baraka toka kwa mola wako...sasa kwanini uichukulie `hivyohivyo tu'....ndio maana mnachokana mapema, kumbe ilitakiwa kila kukicha ndio baaado!
TUPO PAMOJA MPENDWA!

Bila jina alisema ...

jamani hata mimi yameshanikuta hayo kiukweli inauma sana yaani unakuta watu mnaishi kama maadui

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom