Jumanne, Juni 28, 2011

Katika mahusiano ni muhimu kutambua mambo yanayomfanya mtu kuwa na wivu ili uweze kupambana nayo

Wivu unahusika katika mapenzi ya kweli, lakini kumbuka kuwa makini katika hili kwani  kuna baadhi ya watu unakuta mtu ana wivu kwa mwenza wake kwa kuwa na hofu kwamba kuna watu wanamnyemelea au wakati mwingine mtu huyo unakuta yeye ndiye anayemsaliti mwenza wake na wakati huohuo anakuwa na wivu sana kwa mwenza wake kwa kuhisi kwamba yale anayofanya yeye labda na mwenziye anafanya hivyo,

Kuwa makini na mwenza aliye na wivu sana kwako yawezekana anafanya hivyo ili kuficha madhambi yake. jambo la msingi ni kujenga uaminifu kwenye uhusiano ulionao ikibidi hata kupata ushauri kwa wataalamu, ni muhimu sana kwa wote wawili kujifunza namna ya kuwekeana mipaka katika uhusiano na kila mmoja kuheshimu mipaka ya uhusiano wa mwenzake. kadri uaminifu unavyoongezeka ndivyo mnavyotambuana na  kugundua ni vitu gani salama katika uhusiano wenu.

Maoni 4 :

Bila jina alisema ...

ni kweli kabisa Adela haya mambo yapo kwani hata mimi ilishawahi kunitokea mtu anajidai ana wivu mwingi kumbe anamambo yake

Bila jina alisema ...

jamani mimi mpenzi wangu akiwa hana wivu siamini kama ananipenda

Bila jina alisema ...

naitwa Lina wivu ni kila kitu katika mapenzi ila ukizidi ni kero

asu tz alisema ...

Mimi mpenz wng ana wivu hata c elewi nifanye nn? Ahhh

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom