Ijumaa, Juni 10, 2011

Ni vizuri kusamehe na kusahau ili uweze kuishi maisha ya furaha na amani.

Katika maisha inapotokea kuna mtu amekukera inawezekana akawa ni mwenza wako lakini baadaye akakuomba msamaha kwa kile alichokosea kama kweli umeamua kumsamehe basi ni vizuri kujiepusha kuwa na kinyongo yaani ile hali ya kusamehe huku bado moyoni kile kitu unacho kinakusumbua na wakati mwingine labda unayo nia ya kulipiza kisasi au bado unapenda kuzungumzia makosa ya zamani wakati ulishasamehe haipendezi kuwa na tabia ya kutosahau baada ya kusamehe kwani hata wewe mwenyewe binafsi unakuwa hujitendei haki kwani unajidanganya na pia utaendelea kuuumia kutokana na kushindwa kusahau naamini huwa inakuwa ni vigumu kusahau kulingana na uzito wa kosa lakini kama umeamua kusamehe basi samehe kwa moyo wako wote ili uweze kuwa huru na yule umpendaye .

Maoni 5 :

emu-three alisema ...

Hakuna kitu chema kama hicho cha kusamehe, inagawae ni kigumu sana unapokumbuka jinsi ulivyofanyiwa, kwa mfano ulimfuma mwenzako `live'....utawezae kumsamehe mtu kama huyu..lakini ukimsamehe, kwa moyo mmoja, unajua unamweka mwenzako katika hali ambayo `hataweza' kurudia tena labda awe sikio la kufa halisikii dawa!

Simon Kitururu alisema ...

Kwa mtazamo wangu :
Ni muhimu KUSAMEHE!
Ukisamehe unajiondolea mzigo wako piakatika swala.

Ila naamini si vizuri kusahau!

Naamini ukisahau kuna funzo utasahau!

Na ukikosea na kujifunza katika kosa ni muhimu kujisamehe ilimradi usisahau kwa kuwa ukisahau utarudia tu lilelile kosa!

Unknown alisema ...

The Oxford English Dictionary defines forgiveness as 'to grant free pardon and to give up all claim on account of an offense or debt

Majoy alisema ...

Yah ni kweli ukiishi kwa kusamehe na kusahau utaishi maisha ya furaha sana

Bila jina alisema ...

Pole sana dada kwa msukosuko unaokupata kuhusu ndugu zako, mi naona ungetumia busara usifanya hasira hautamaliza tatizo, jaribu kuwaita wazee au viongozi wa kidini uwaeleze wamuite wajaribu kuongea nae na kumwelezesha maana kuoa au kuolewa haina maana kwamba tusiwasaisie ndugu au jamii inayotuzunguka si vema kwa kuwa shida huwa inaweza kumtokea mtu yeyote na mahali popote katika hali yoyote kwa hiyo hata kama mko kwenye ndoa ninyi pia mnaweza kupata tatizo au matatizo na mtahitaji watu wawasaidie, swali kama hamtawasaidia wengine ninyi mtasaidiwa na nani?na hata msipopata tatizo kwa ujumla watu tunatakiwa kusaidiana, huyo ana matatizo sasa yeye ndugu zake pia hawasaidii au wa upande wako tu anahitaji kusaidiwa kwa ushauri na zaidi sana maombi, jipe moyo usikate tamaa.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom