Jumatano, Juni 08, 2011

"Wazazi wangu hawamtaki mchumba wangu"

Nimepata ujumbe huu leo kutoka kwa James mkazi wa Kimara Dar es salaam. Mimi ni mwanamume nimezaliwa  katika familia ya watoto wanne nikiwa ni mtoto wa kwanza katika familia katika maisha yangu baada ya kumaliza masomo ya chuo nilipata mchumba ambaye ninampenda sana na nia yangu nikuja kufunga naye pingu za maisha tatizo ni kwamba hivi majuzi nilimtambulisha mchumba wangu kwa wazazi ambapo kiukweli hali haikuwa kama nilivyotarajia.

  Baada ya kuondoka yule mchumba wangu baadaye baba na mama waliniambia kuwa hawampendi huyo mwanamke niliwauliza tatizo ni nini wakasema anaonekana hajalelewa katika maadili mazuri,,na hata kabila alilonalo hawakulipenda kiukweli mimi binafsi nampenda sana mchumba wangu na sitaki kumuacha tatizo linakuja wazazi wangu wanasema iwapo nitaamua kumuoa huyo msichana basi nisahau kama wao ni wazazi wangu inaniuma sana kwani naamini mambo ya kuchaguliana mchumba yamepitwa na wakati  sijui nifanyeje ili wazazi wangu wamkubali mchumba wangu,,,,,,,,,,

Maoni 7 :

Hashir alisema ...

Ukisikia maumivu ya mapenzi ndio kama hayo!! Ila mimi ningependa kumshauri huyo kijana kwamba wazazi ndio wazazi, na wanabidi wapewe nafasi yao katika maisha yakila siku, ajaribu kukaanao vizuri na kuzidi kuwaomba kwa njia moja au nyengine, pia ajaribu kumtuma mtu ambae anahisi atakuwa rahisi kusikilizwa na wazazi wake, labda patapatikana suluhishi. Lakini pia, akumbuke kwamba ndoa zote hapa duniani zipo mikononi mwa Mungu, ukiona ndoa imefungwa, basi ujuwe Mungu ameridhia, kwahivyo kama wanapendana sana, na roho yake inaumia kumkosa huyo mwanamke kwa sababu ya wazee, basi amrudie Mungu. Kama hiyo ndoa ataifunga kwa ujasiri wa kutoogopa maneno ya kususiwa na wazeewake, basi ajuwe hiyo ndoa imefungwa kwa uwezo wa Mungu, wazee hapo watakuwa hawana nafasi mbele ya Mungu, so yeye atabaki kutafuta njia za kurudisha amani baina yake na wazee wake, lakini ajuwe mbele ya Mungu atakuwa hana dhambi na ndoa yake ni halali. "Pole sana, coz naamini uchungu wa mapenzi unazidi uchungu wa mwanamke wakati anapozaa"

Rik Kilasi alisema ...

Duuuh!!!! Kaka James kwanza nikupe pole maana hio kitu ni ngumu sana wazazi kufikia kutoa kauli hio inawezekana wamewaza mengi kama sio kumjua binti mwenyewe.Ila siku zote msimamo wako ndio kitu cha msingi zaidi coz huyo mwanamke wewe ndio utaishi naye na sio wazazi wako kwa maana hiyo ni jukumu lako kuwaelewesha kua huyo ndio chaguo lako kwa sasa na si vinginevyo.

Nasema hivo kwasababu kama kweli unampenda huyo binti na ukamuacha kisa wazazi basi ukimpata mwingine huta mpenda kama huyo na huo ndio mwanzo wa kuchokana mapema na hata kua na nyumba ndogo...Si hivyo huyo binti nina hakika hujawa nae leo wala juzi ni wa muda so ushampotezea muda (kama utaunguna na wazazi) masikitiko ya hawa watu(mabinti kama sio wanawake) hua yana laana za ajabu sana mifano ipo mingi katika jamii..

Cha kujiuliza ni je wewe una mapenzi ya kweli na huyo binti? je una uhakika kama huyo binti anakupenda kiukweli sio msanii? Hii ina maana ikiwa hakuna mapenzi ya kweli na ikaja tokea tatizo utakacho ambiwa ni kua ''uliona sisi hatuna akili tulipokuambia hakufai?'' kwa maana nyingine ni kwamba ukiwa na tatizo na huyo binti ambaye kwa muda huo atakua mkeo basi hutakua na uhuru wakushirikisha wazazi!

Mwisho kabisa ikiwa utaamua kumuoa huyo binti bila ridhaa ya wazazi ni lazima uhakikishe huyo binti hajui kama hapendwi na wazazi coz akijua tu na vile wazazi hawampendi visa havita isha kwa pande zote mbili na hatimaye ugomvi wa mara kwa mara hapo ndipo ndoa inapo kua chungu wenyewe wanasema ndoa ndoano.

Nihayo tu kwa leo mwana kimara mwenzangu nakutakia kila lakheri katika huo mchakato....

Bila jina alisema ...

kaka we inabidi uwasikilize wazazi kwani wao ndio walio kuweka duniani, wao wanajua baya na zuri.naitwa john cosmas tbt.

Bila jina alisema ...

siku hizi hakuna kuchaguliana mchumba mimi nakushauri umuoe hao azazi waache ushamba

Bila jina alisema ...

hata mimi ilishawahi kunitokea ilinichukua muda mrefu sana kukubaliana na hali halisi kwani niliamua kuwasikiliza wazazi wangu ila baadaye nilijuta kwani nilikuja kuoa mwanamke ambaye sikuwa na mapenzi naye ilinisumbua sana hivyo kujikuta tumeachana mimi nakushauri utulize akili usifanye maamuzi ya haraka kuwa makini naitwa John

Bila jina alisema ...

Kwa vile ulimpeleka huyo mpenzi wako kwa wazazi ili wakamuone na waridhie, basi ujue kuwa nafasi yao kama wazazi waliitumia vizuri sana kumchunguza huyo binti kwa muda mfupi tu aliokuwa hapo kwao. Japo wengine wanasema hakuna kuchaguliwa wachumba,lakini kumbuka kuwa hakuna anayempita mzazi.Muhimu mimi nakushauri endelea polepole kuwekana sawa na wazazi bila hasira wala fujo ili muelimishane na yamkini utakuja pia yaona hayo wanayozungumzia kama ni tatizo au wao wakaelewa kuwa hayo walioyaona muda mfupi si tatizo.
Wazazi ni muhimu mno mtu asikudanganye,hata kama si wao utakaoishi nao lakini ndiyo watoao baraka kwa watoto wao ukiacha baraka lukuki toka kwa Mungu maana Mungu amesihi waheshimu baba na mama yako ili siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Mungu.Kwa hiyo endelea kushauriana na wazazi taratibu ili wakuelewe na wewe uwaelewe vema.

Nakutakia kila la heri.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom