Jumatano, Julai 06, 2011

Anaomba ushauri "Nina ujauzito lakini naogopa kumwambia muhusika kwasababu hatujawahi kupanga kama tutakuja kuoana nahisi anaweza kuniacha....

Habari zenu wapendwa niko hapa kwa ajili ya kuhitaji ushauri kutoka kwenu mimi ni msichana wa miaka 3o nakadhaa ni mdau mkubwa wa blog yako. Naomba niende direct kwenye point… nilikuwa nipo na mwanaume mmoja tulipendana  ila alikuwa na tabia Fulani hivi ambazo mimi niliona sitaweza kuwa naye na tulidumu kwenye uhusiano kama mwezi nikaamua kukata mawasiliano naye but yeye alijitaidi kunitafuta kwa kipindi chote na kufanikiwa kunipata  na kila akitaka kukutana na mimi ili tukae chini tuongee ajue ni nini kilisababisha mie kukatisha mawasiliano nilikuwa najidai niko busy.


Basi ikafika kipindi alichoka na kuamua kuanzisha uhusiano na gal mwingine ambaye hawakudumu sana yule gal akamwibia na kutoroka nchini, akarudi kwangu tena kwa mara nyingine mimi nikawa nipo kwenye mahusiano na boy mwingine nikamueleza akapata tena demu ambaye alipanga kuwa atamuoa but yule gal akakataa kuolewa naye na kumuambia ana ujauzito wa mtu mwingine sio yeye. Wakati yeye anapatwa na hekaheka hizo mimi nilikuwa nimemfumania boyfriend wangu na gal mwingne nikaamua kuachana naye. Ukumbuke kipindi hicho tulikwa tuna mawasiliano ya kama marafiki basi tukaja tukakutana na kila mtu kueleza wapi amenipitia na kuamua kurudisha tena penzi kama mwanzo na kukubaliana kuwa tukae kwanza mpka kila mtu atakapoona kuwa anaweza kuishi na mwenzak tukaenda kupima VVU ili tuwe huru.


mwaka jana tukaanza kukiss each other ambayo ilitupelekea tukafanya mapenzi tukaendelea hivyo mpaka sasa nikiandika hapa hatujawahi kukaa na kuongea labda tutakuja kuoana na badala yake huyo mwanaume aliwahi kuniambia kuwa nikipata mwanaume au nikimpenda nimueleze na  akitaka kunioa nimwambie. Ninaombeni ushauri wenu  maana sasa hivi mimi ni mjamzito wa wiki sita je nimwambie kuwa mimi ni mjamzito? Na mimi kutoa mimba sitaki maana ni sawa nakuuwa kiumbe kisichokuwa na hatia na siwezi jua labda mungu ndio kanipa yai hilo moja na mie nikitoa itakuwaje, na kumueleza kuwa ni mjamzito naogopa.  Je nifanyeje?

NB nimetoka familia ambayo ni ya wacha mungu na mimi huwa wakati mwingine nahudumu kanisani najisikia vibaya maana nitakuwa nimewadhalilisha wazazi wangu na mie nitatengwa na kanisa. Je wadau nifanyeje??????

Naombeni ushauri  sio kunipa madongo. Poleni kwa mail ndefu ya kuchosha

Maoni 7 :

Hashir alisema ...

Kwanza kabisa hapa ndio tujuwe mapenzi hayana umri, unaweza ukawa na umri mkubwa ila bado ukawa unatawaliwa katika hisia na akili yako kwa nguvu ya mapenzi (mapenzi hayana ukubwa jamani). Pili niende katika point, mimi nimeisoma hiyo stori ya huyo mdada vizuri sana, yaani kwa maelezo yake tu yanajitosheleza kuona kwamba huyo mwanaume hafai kabisa,,, haiwezekani uwe na demu, halafu eti umwambie kama akipata mwanaume au akitokea mtu anataka amuoe, akwambie ili umruhusu aolewe...khaaaa!!! sasa hapo kuna mapenzi kweli,,, huyo mwanaume aachanenae, asije akapata matatizo zaidi ya hayo aliyopata,, kama alivyo sema kwemye blog kwamba yeye ametoka katika familia ya wachamungu, basi na hiyo mimba aliyonayo pia imetoka kwa Mungu, so haina haja ya kuitoa, chakufanya ni kuamuwa kutubu na kuomba kanisa limrudishe kundini...ila mwanaume huyo hafai kabisa!!

Bila jina alisema ...

maji yakishamwagika hayazoleki ndugu yangu ni bora umwambie ukweli kwani hata ukikaa kimya haisaidii chochote

Bila jina alisema ...

heee huyo mwanamume alikuwa hajatulia hata kidogo yaani alikuambia ukipata mwanamume olewa tu yaani ungetakiwa uwe makini tokea mwanzo mdogo wangu ila hauna namna wewe mueleze ukweli kuhusu ujauzito hata akikataa wewe mlee tu mwanao

Bila jina alisema ...

pole sana dada ila kuwa makini na huyo jamaa mwambie tu ukweli haina haja ya kuogopa mimi naitwa Obed

ADELA KAVISHE alisema ...

ushauri kutoka facebook

Mary Mushi... Jamani Adella, hapaswi kuogopa kwa nini uogope naye ni muhusika, mwambie ukweli.
about an hour ago · Like

Joseph Masaga... ‎@Adella hapo nikupoteza mda some time mtu anamiaka 30 mmsitoi coments kwake kwa sbb alikuwa anatenda tendo la ndoa bila kinga na ujue huyo mwanaume alijua kitendo bila kinga kinachofuata ni ukimwi magonjwa hatari au mimba so alijipanga kwa lolote so me ningesikia mwanaume kanipa mimba kaniacha ningechangia hoja but kila mtu na mtazamo wake

Vinens Rizzy William.. Muhusika amwambie tu, mimba c kifo!


Moses Lodoviki... MWIBA WAKUJIDUNGA MTU AMBIWI POLE, MAMBO MAWILI AKOME AU AZIDI

Ahmed Maulid.... we usijali mwambie tu, kama akimkataa mtoto basi naomba uniletee mm, 7bu mm nataka mtoto lakini sijapata.

Bila jina alisema ...

kwan wakat mkido pekupeku mlitegemea nini?au alijua huna kizazi? au yeye hana mbegu za ku2nga mimba?mweleze ukwel ana haki ya kujua results za matendo yake and he has to be responsible ,you as well-lucy

Bila jina alisema ...

Tell the guy the truth don't judge him and if he will say no let him go don't force to stay where you don't belong it will cost you a lot in your life. Tell him so that you will ready to start your life without him by your side.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom