Jumanne, Agosti 23, 2011

mimi ni msichana naombeni ushauri,mpenzi wangu nampenda lakini nimegundua anamwanamke mwingine ambaye anaishi mbali

Jamani naombeni ushauri kupitia blog ya Adela mimi ni msichana nina mpenzi wangu nampenda sana hivi majuzi nilichukua simu yake kuangalia phonebook nikakuta kuna mwanamke amemuandika kwa jina la My lover nilistuka na kuangalia mimi ameniandika kwa jina gani nilkakuta ameniandika mpendwa,, nilichukia sana na kutaka anipe namba ya huyo mwanamke eti ananiambia hawezi kunipa kwasababu nitagombana naye na huyo ni mchumba wake anaishi huko mikoani inaniuma sana kiasi kwamba nimemuambia tuachane yeye ananiambia hawezi kuniacha ananipenda na ana wivu sana kwangu hivi huyu mtu ananipenda kweli jamani ????

Maoni 6 :

Regan Mbare alisema ...

Pole sana wewe dada kwa yaliyokukuta. Ila mustakabali wa maisha yako uko mikononi mwako sio kwa mtu mwingine.

Kama umefanya uchunguzi wa kutosha na kujua kweli huyo jamaa ako anamtu mwingine na wanakutana na kushiriki mapenzi inabidi uchukue maamuzi yaliyo sahihi kwako, ama kukubali kuendelea naye au kuachana naye uendelee na maisha yako.

Pia inategemea kama mlianzaje mahusiano yenu na kwa kiasi gani mlikuwa wazi kwa kila mmoja kuhusu mahusiano ya nyuma kabla hamjakutana. Kama mlifichana hayo ndio matokeo yake.

Ila katika yote uamuzi unao wewe kwani hata kuwa naye ni wewe uliyekubali baada ya yeye kukutongoza, labda kama ulimtongoza wewe itakuwa tofauti.

Bila jina alisema ...

pole sana dada yangu,najua uko kwenye wakati mgumu sana kwa hilo lililokukuta mama coz am woman to ambaye nimepitia hayo pia so naju sio rahisi kumuacha mtu unayempenda ingawa inawezekana kwa sababu yeye sio mungu mpaka ushindwe kuishi bila yeye dada yangu.


mi nakushauri uachane nae huyo jamaa coz kama amekutamkia kabisa kwamba huyo dada ni mchumba ina mana tayari anaye mtu wa maisha yake na sio wewe anakupotezea muda tu na kukuzeasha ili upite umli wa kuolewa kisha akucheke mama yangu.kimbia ile mbaya sio mwanaume mzuri kwako ni mwanaume mzuri kwa huyo dada mwingine mama yangu open your eyes and see and then act.

Bila jina alisema ...

ila wanaume wa kibongo sio wa kupenda sana coz ni wadanganyifu sana soo achana nae kama ameadimit kabisa anaye mwingine it means wewe hakupendi mama yangu acha kujidanganya et kwa vile anakuonea wivu na kusema hawezi kukuacha eti ndo anakupenda sio kweli wanaume ni waongo sana si wa kuamini ni muongo huyo.siku muda wake wa kuondoka ukifika atakuacha bila huruma huyo na kwenda zake na kama unabisha subiri yakukute mama yangu ndo utaamini

Bila jina alisema ...

pole sana dada yangu hata mi yalinitokea hayo tena hivo hivo kama wewe unajua nilimuambiaje,nilimuambia hivi du u luv,alijibu ndio,nilimuuliza tena du u nid mi in your life alijibu ndio,basi nilimuambia ampigie simu huyo mwanamke mbele yangu kisha amwambie ana mwanamke mwingine ambaye ndo mi kisha kama yuko tayari atuoe wote na tujuane.bwana we hapo ndo nilipoona upendo wake kwangu alishindwa kufanya hivo.so jaeibu kufanya kama mimi kisha uone dada.sidhani kama unaweza kuishi au kuwa na mwanaume unayejua hakupendi na wala hana mpango na wewe naamini utakuwa chiz kama jibu lako ni ndio.take kea jithamini na jipende.usikubali kuchezewa akili

Bila jina alisema ...

mmh pole sana mapenzi ya siku hizi hakuna uamnifu kabisa. Sasa mpendwa huyo ameshakwambia kuwa huyo ni mchumba wake inamaana wewe ni nani? Funguka mpenzi

Bila jina alisema ...

Sasa dada unataka jibu gani tena..wewe anakupenda kama MPENDWA WAKE na huyo uliyekuta kwe cm ndo HIS LOVER..sasa hapo inahitaji formular na calculator kucalculate. Hicho ulichokikuta ndo ukweli uliopo moyoni mwake, he is in love with someone else and not you, wewe ni wa muda tu kutuliza tamaa zake wakati mpenziwe yuko huko mkoani. so JIPE MOYO,AND MOVE ON......pole kwa ushauri mkali lkn sipendi kuumizwa, so i feel sorry kwa girls wenzangu wanaoumizwa, NASHANGAA unasubiri nini hapo.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom