Jumatatu, Septemba 19, 2011

Namna ya kumbadilisha mpenzi kutoka kwenye tabia mbaya na kwenda nzuri.

a
Katika mahusiano ni jambo ambalo linawezekana kwa mwanamke au mwanamume kumbadilisha mwenza wake kutoka tabia mbaya kwenda nzuri lakini ni muhimu kuzingatia yafuatayo, unapotaka kufanya jaribio la kumbadilisha tabia mwenza wako usijenge hoja za kumkosoa na badala yake anza kwa kumsifia yale mazuri aliyonayo kwani kwa kufanya hivyo kutamsaidia huyo mpenzi wako kuanza zana ya kujielewa yeye ni nani ,,kwa mfano kama mpenzi wako ni mlevi ukawa unatumia lugha kama kumkebehi na kumdhalilisha mbele za watu ukifikiri kuwa atabadilika inakuwa ni vigumu kwani inawezekana ndiyo kwanza akazidisha.

kinachotakiwa ni kumwambia kwa lugha tamu kuwa mtu kama yeye ambaye ana nguvu na mvuto hapendezi kulewa ,, taratibu ataanza kujielewa na mwisho atapunguza kabisa kama si kuachana nayo, kutumia changamoto za kukosoa kulaumu au kukaripia kama sehemu ya kumfanya mtu kubadilika tabia hakutasaidia mtu kubadilika na inawezekana akaongeza zaidi.tumia lugha tamu kumbadilisha umpendaye.

wengine wanakwama kutokana na kukosa hoja za msingi za kupinga tabia ya mtu na hii inatokana na kutokujiamini ama kusimamia maamuzi wanayotoa dhidi ya wapenzi wao lakini pia ni vyema kuelewa mtu atabadilika pale tu atakapokuwa na ushawishi wa kutosha kwamba mabadiliko anayopaswa kufanya yatakuwa na faida kwake na si vinginevyo

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom