Jumatano, Oktoba 19, 2011

Inawezekana mtu akawa analazimisha mapenzi bila kujitambua kuwa anafanya hivyo

Mapenzi ni maelewano baina ya wawili wapendanao kukiwa na uaminifu na upendo wa dhati ndani yao na huku kila mmoja akiwa anampenda mwenza wake kutoka moyoni ikiwa ni katika hali yoyote ile, iwe shida ama raha,,lakini inapotokea mmoja anampenda mwenziye zaidi basi ujue kuna tatizo ni vyema kutambua uhusiano ulionao je kweli niliyenaye ananipenda ama kuna kitu anakipenda kutoka kwangu au anajilazimisha kunipenda ili apate faida fulani?? 

Ukweli ni kwamba ni muhimu kutafakari kuhusu hilo na wewe binafsi kutambua je kweli huyu mtu ninampenda au najilazimisha kumpenda,,kwani naamini mapenzi ya kulazimisha siyo mazuri hata kidogo mwisho wake utajuta kwa nini sikujitambua mapema,

Inawezekana mtu akawa analazimisha penzi bila kujitambua kwasababu ya mapenzi aliyonayo kwa yule anayempenda kwa mfano anaweza kumthamini kwa kumpa mali ama kila kitu anachohitaji yule anayempenda bila kujua je huyu ninayempa hivi vitu ana mapenzi na mimi kwa kufanya hivyo unaweza kuumia sana moyo wako hapo baadaye uliyemjali na kumpenda ukafikiri ni wako kumbe hana muda na wewe. NI VYEMA KUJITAMBUA MAPEMA

Maoni 5 :

Bila jina alisema ...

yaani Adela hapa umenigusa mimi nahisi huwa nalazimisha kuna mtu nampenda lakini huwa simuelewielewi hata kidogo

Bila jina alisema ...

hiii ni kweli jamani mambo ya kulazimisha usipopendwa ama usipopenda huwa haipendezi na utajuta baadaye

Bila jina alisema ...

UKO SAHIHI KABISA ADELA NI BORA SOONER UNAPOGUNDUA U A JUST FORCING NO LUV BETWEEN U BETA STOP IT TENA KIMBIA KABISA WE MWANAMKE MWENZANGU

Bila jina alisema ...

hata mimi adela umenigusa sana naamini nami ndo hivo hivo kama mdau hapa juu usijali mamaa kama tayari umeshagundua hilo jitahidi kutoka kwenye hayo mapenzi ya ajabu usilazimishe penzi utakuwa unapoteza muda wako tu kimbia kabisa utaidhurumu nafsi mpaka unakufa u cant buy luv for materials muombe mungu kila siku akunyooshee mambo yako kikazi na akupatie atakaekupenda mama yangu achana nae coz kila unapomng'ang'ania huyo asiyekupenda ndio unasiba nafasi kwa anayekupenda au atakaekupenda kwa dhati

Simon Kitururu alisema ...

Mapenzi sio maelewano !Mkielewana yapendeza lakini MAELEWANO ya kutumia akili sana ni maelewano kwa kuwa munawazua nijinsi gani mlee muitacho penzi lakini PENZI lakutumia akili labda si PENZI na ndilo machuna buzi walitegemealo kwa JINA tu.

Ndio,...
... labda MAPENZI ni maelewano lakini kuelewana NIMCHEZO tofauti kabisa hasa kwa kuwa hakuna watu wawili SAWASAWA na ndio maana kama umependa na kwa kupenda kwa dhati umejikuta unalazimisha mtu,...
... kwangu hilo lasameheka kwa kuwa nni kitendo kutoka moyoni. Lakini KUELEWANA ili liwe penzi kisa nishastukia udhaifu wako na naishi kikutokuwa mimi ili uendelee kujigonga au kudhani unapendwa ... labda hilo si PENZI!

nawaza tu kwa sauti!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom