Jumanne, Oktoba 11, 2011

Mke wangu anatabia ya kuwatukana wafanyakazi wa kike sehemu ninayofanyia kazi kwa madai kuwa natoka nao kimapenzi,,,,,,

Habari yako Adela pole na majukukumu mimi ni mwanamume nina mke na watoto watatu nampenda sana mke wangu na watoto wetu tatizo ni kwamba mke wangu anawivu sana yeye ni mama wa nyumbani lakini mimi nafanya kazi na katika kampuni ninayofanya kazi wanawake ni wengi kutokana na ushirikiano wa kazi na wafanyakazi wenzangu mke wangu amekuwa na tabia ya kuchukua namba za simu zenye majina ya wanawake na kuwapigia simu huku akiwatukana nimejaribu kumkanya hiyo tabia inashindikana inafikia kipindi mimi nagombana na wafanyakazi wenzangu huku wakihisi mimi ndiye ninayempa mke wangu namba zao hii tabia inanikera NAOMBENI USHAURI JAMANI

Maoni 4 :

Simon Kitururu alisema ...

Wivu katika usemalo misingi yake mikubwa ni kutojiamini kwa mwenye wivu huyo mkeo.

Jaribu kujua kwanza ni kwanini anawasiwasi ataibiwa! Bila kujua siri ya kukosa amani kwake mbele za wanawake wengine hutaweza kutatua swala hili. Na kabla ya hapo usiweke namba za wanawake kwenye simu yako hasa kama sio muhimu kihivyo...
Kumbuka mambo ya simu yamekuja juzijuzi tu na wivu pamoja na mapenzi kati ya mke na mume yapo tokea zamani. Jaribu kupiama kama kuwa na namba za wanawake wengine hata kama ni wafanyakazi wenzako na NDOA yako ni nini ni muhimu zaidi. Na kama ni muhimu NDOA , futilia mbali namaba za watu au hata acha kuwa na simu kabisaa.

Pili nahisi mke wako anamuda mwingi kupita kiasi! Mtafutiekazi hata kajibiashara apunguze kuwa na muda wakufikiria vyakufikirika. Unajaua tena muda mwingi ukimpa mtu kufikiria vitu hata vya uongo, uongo huanzageuka kuwa kama KWELi vile!:-(

Ni mtazamo wangu tu !

Bila jina alisema ...

umesema kweli simon kitururu umemaliza yote niliyotaka kusema kumbe saa nyingine unabusara maana saa nyingine nikitembelea blog yako nakuta pumba tupu mpaka nikawasiingi ktk blog yako mara uandike matusi huwaga sisoma blog yako tena lakini leo umeandika point naona unakuwa sasa

Simon Kitururu alisema ...

@Anony: Kwa bahati mbaya Blogu yangu iko vilevile na NIKO VILEVILE kifulu PUMBA na sijabadilika. Kuna uwezekano nimebahatisha hapa !:-(

Bila jina alisema ...

Sasa wewe simu za wanawake wa kazini ktk sim yako zinafuata nini?

Unayataka mwenyewe,

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom