Habari Adela pole na majukumu ya kila siku mimi ni mwanamke nimeolewa nina watoto wanne maisha yangu na mume wangu mwanzoni tulikuwa tukiishi vizuri ila kwa takribani kama mwaka mmoja sasa mume wangu amebadilika sana kila kukicha napigwa bila sababu kila nikimuuliza akichelewa kurudi ananipiga sana na wakati mwingine ananitafutia sababu zisizo na msingi huku akiniambia kuwa atamleta mwanamke mwingine ukweli mimi natamani kuondoka lakini watoto wangu nawaonea huruma kwani nawapenda sana nikiondoka hawatapata malezi bora sijui nifanyeje kuhusu hii tabia ya mume wangu
Maoni 4 :
kwani wewe ndio mwenye mallezi bora kuliko wanawake wengine?
Kwani wewe ndio wawapenda kuliko mtu yeyote?
Kwakutaftiwa visingizio hilo nakataa kwanza tuambiye your side sio tu ati yuanitaftia visingizio kumbe chanzo ni wewe kwa mambo yako unayoyaficha. Kama hujui sababu ya yeye kubadilika jiulize ulikuwaje awali na sasa ukoje.
Ulimshirikishaje awali na sasa niaje?
mwanamume anaepiga,si mwanamume.jee umewashirikisha ndugu na kuwaeleza?ukiendelea kukaa utapata kilema bure kwa ajili ya vipigo.yakiendelea,ruuuuun as fast as you can.najua ni ngumu sana kama una watoto
Hapa nadhani tatizo ni kuwa umechokwa na kuna mwanamke mwingine!
Na anakubwenga kwa kuwa hajui akufukuzeje .
Jichunguze nini hakinogi sikuhizi.
Na kumbuka kwa kupigwa unaweza ukapigwa mpaka ukauawa au kulemazwa kitu ambacho kwa watoto wako kitakuwa kibaya zaidi ya kwako kuwa hai na kuishi bila huyo MUME akutesaye huku angalau wana MAMA wa kumkimbilia.
Ni mtazamo tu hasa kwa kuwa hujasema mengi ili tujue picha nzima ili tudadavue kiini cha tatizo ni nini.
Nakuonea huruma wewe na watoto wako.
Kama haumpendi timua zako tena chukua na watoto wako.
husikubali watoto wako walelewe na mama wa kambo watanyanyaswa na kuaribika.
na muambie hautaki watoto wako wanyanyaswe na malaya wake atakae mleta, ndio maana upo hapo kwa ajiri ya watoto wako. Akikuambia ondoka chukua na watoto wako, basi ondoka nao.
Kama unampenda mumeo basi
mkalishe chini mwambie karogwa na hao malaya wake, ili akunyanyase wewe, ndio maana kabadilika.
Maisha ya kupigwa sio mazuri, na watoto kama wanajua unapigwa sana watakuwa wanaumia sana ila hawana la kusema. Watakuwa wanaishi maisha ya unyonge. Na ugomvi wenu utaaribu watoto wenu, bora ukimbie kalee watoto wako kwa amani peke yako. Bora umaskini na amani, kuliko utajiri na manyanyaso
Chapisha Maoni