Jumatatu, Novemba 28, 2011

"Ameolewa lakini bado anataka tuendeleze mapenzi ya kimya kimya"

Habari yako Adela kwanza hongera kwa kuwa na blog nzuri ya kuelimisha jamii, mimi ni mdau wako na pia nina matatizo yanayonisumbua katika mapenzi nilikuwa na mpenzi nilimpenda sana tumekuwa katika mahusiano takribani miaka mitatu lakini baadaye mwenzangu aliolewa kwa shinikizo la wazazi wake, niliumia sana kwasababu nilikuwa nampenda.

wakati huo mimi nilikuwa sijapata kazi ndiyo nimemaliza elimu ya chuo baada ya yeye kuolewa alikuwa na maisha mazuri sana kwani mume wake ni mtu mwenye uwezo kifedha, tulikuwa tunawasiliana akaahidi kunitafutia kazi kutokana na shida nilizokuwa nazo nilikuwa tayari kufanya kazi mahali popote ndipo aliponitafutia katika kampuni ya mume wake.

Ukweli ni kwamba kazi ni nzuri na mshahara napata mzuri lakini tatizo  ni kwamba huyu mwenzangu bado anahitaji tuendeleze mapenzi kimyakimya na anaoenyesha wivu hata kwa baadhi ya wanawake ninaofanya nao kazi, inanipa wasiwasi sana nilishawahi kumuambia mimi na yeye haiwezekani kuwa wapenzi  tena namuheshimu sana.

Lakini naona mwenzangu anakasirika ananitafutia visa kiasi kwamba nahisi ataniaribia kazi na mimi kazi yangu naipenda kwani ni msaada mkubwa kwa familia yangu, wazazi wangu wanaonitegemea naombeni ushauri wenu jamani kupitia blog hii ya Adela

Maoni 9 :

Bila jina alisema ...

kaka kama unapenda maisha yako mi nakashauri tafuta kazi sehemu nyingine au mkoa mwingine la sinyo huyo mwanamke akishaona imeshindikana kurudiana nae anaweza hata akakuzulia uongo wowote kwa mmewe ambae wewe ni bosi wako na kukuharibia. sio tu kazi kaka yangu hata uhai wako pia.

Bila jina alisema ...

Me nakushauri jaribu kumuelewesha kuwa yy ameshaolewa so c vzr kuendeleza mahusiano n kweli mwanzo mnaweza kumudu kufcha fcha but at the end of the day mumewe atakuja kujua hapo ndo balaa litaanza, kaa mbali na huyo mwanamke km hataki kukuelewa tafuta kaz shm nyngne pia kata mawasiliano nae.

Joh...

Bila jina alisema ...

KWANI WEWE HUKUJUA KAMA HUO MWANAMKE ALIKUWA BADO ANAKUPENDA NDO MANA AKAHANNAIKA KUKUTAFUTIA KAZI KWA MUME WAKO AU UNAJIFANYA HUKUJUA UKADHANI NI MAMA YAKO HUO ANAKUHANGAIKIA.UTAKUFA KAKA KWANI HATA WEWE UNAWEZA KUMUHANGAIKIA MKE WA MTU AU MWANAMKE YOYOTE BILA REASON YOYOTE AU UNAVUNGA KAKA.FANYA UAMUZI WA KUTOKA HAPO KABLA MAMBO HAYAJAHARIBIKA SHAURI YAKO WE ENDEKEZA SHIDA TU MATOKEO YA NJAA UTAYAONA.

Bila jina alisema ...

Tafuta kazi sehem ingine, na acha kazi. au jifanye unaumwa, na uwezi kazi tena, ili boss na mwanamke wasikuaribie future

jigambe alisema ...

Ebwana kaka unamtihani mkubwa sana but kama alivyosema mtazamaji hapo juu tilia maanani hilo swala! thank at www.jigambeads.com and tanzaniakwetu.com ni vyema kuisajili hii blog ili ijulikane na ipate matangazo zaidi!

Bila jina alisema ...

Sio mama yako huyo.kama vipi unapenda maisha yako kama mdau hapo juu sepa.

Bila jina alisema ...

Mwanaume mwenzangu, we endelea kula nyapu kama yeye yuko tayari piga, na kula lakini uwe makini sana na umwambie huyo bibie mhakikishe mnafanya kwa siri kubwa na msifuatanefuatane popote ambapo watu watawashuku.nadhani kuna kitu anakikosa kwa mumewe katika suala zima la mapenzi hivyo kukumbuka jinsi wewe ulivyokuwa unampa mapenzi matamu.

Uwe msiri ingawa wansema siku za mwizi ni arobaini, lakini ukiwa makini sana utayaweza maadamu demu mwenyewe ndiye mwanzilishi atajua kuifanya siri hiyo vizuri.Anachotaka huyo ni kutiwa tu na mchezo ukiisha basi anarudi kwa mumewe.Na ukiendelea naye, uwe pia unatafuta kazi mahali pengine ili ukipata tu unaachana naye kabisaa, ila kwa sasa tunza kazi yako kwa kumpa penzi huyo bibie usije kukosa vyote.

Bila jina alisema ...

Akili kwa kichwa kaka.We pima maushauri uliyopewa kisha amua utakavyoona sawa wewe.Hope wewe sio mtoto ila unapingana na ukweli.Ila ninanyojua jua mimi hata wanaume mnachukiana kwenye mafanikio ndo mana huyo mkaka hapo juu amekushauri alinyokushauri ila mi sikubaliani nae coz hakutakii mema.Pima maneno yake huyo mwanaume mwenzako kisha chekecha akili na umsome kama anakutakia mema au mazuri kaka.kila lakheri.

Bila jina alisema ...

mke/mume wa mtu sumu!nakushauri tafuta kazi sehemu nyingine huyo mwanamke atakuponza kwanza angekua na mapenzi ya dhati na wewe asingeolewa japo angelazimishwa lkn alikuona huna kitu akaolewa na
Referer: http://www.blogger.com/commentyomgonga tu si kingine.kuwa makini kaka unategemewa ww kesho akuzushie la polisi ukasote segerea kisa umasikini .chukua hatua ndugu yangu.pole!!!!!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom